Home LOCAL MARUFUKU KUTUMIKISHA WATOTO KWENYE MACHIMBO-MAJALIWA

MARUFUKU KUTUMIKISHA WATOTO KWENYE MACHIMBO-MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Februari 13, 2023 ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Songwe ambapo akiwa katika kijiji cha Kaloleni kata ya Mkwajuni ameweka jiwe la msingi la hospitali ya wilaya ya Songwe.

Ujenzi wa hospitali hiyo ambao umegharimu shilingi bilioni 3.5 mpaka sasa imefikia asilimia 95 ya ujenzi wake ambapo Halmashauri inatarajia kukamilisha Mradi huu tarehe 31 machi 2023, ikiwa ni sambamba na kuanza kutumika rasmi kwa majengo yote ambayo tayari vifaa vyake vimepokelewa.

Ujenzi katika hospitali hiyo inahusisha Ujenzi wa Majengo ya huduma za wagonjwa wa nje, Mionzi, Maabara, ufuaji, Famasia, Utawala na Jengo la Mama na Mtoto, Ujenzi wa Wodi tatu za Magonjwa Mchanganyiko.

Majengo mengine ni jengo la Huduma ya dharula na Nyumba ya Watumishi Familia tatu, jengo la Upasuaji, jengo la Uchunguzi na kuhifadhia maiti na wodi mbili za Upasuaji (Wanaume na Wanawake)

Previous articleWANANCHI 904 WANUFAIKA NA MFUKO WA TASAF MANISPAA YA MUSOMA, WEISIKU CHACHA YEYE AMEJIKWAMUA KWA MATUNDA NA UFUGAJI NG’OMBE
Next articleKAMPUNI YA TANZANIA DISTILLERIES LIMITED YAZINDUA KONYAGI AINA YA KONYAGI FUSION
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here