Home LOCAL WAZIRI UMMY AWAAGIZA WENYEVITI, WASAJILI KUWACHUKULIA HATUA WANAOKIUKA MAADILI.

WAZIRI UMMY AWAAGIZA WENYEVITI, WASAJILI KUWACHUKULIA HATUA WANAOKIUKA MAADILI.

Na. WAF – Dodoma

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amewaagiza Wenyevyiti na Wasajili wa Mabaraza na Bodi za Kitaaluma nchini kuwachukulia hatua kali wanataaluma wanaokiuka maadili ya taaluma zao ili kuilinda jamii na huduma zitolewazo.

Hayo yamesemwa Januari,17, 2023 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha pamoja na Wenyeviti wa Mabaraza ya kitaaluma na Bodi za ujasili zilizo chini ya Wizara ya afya kilichofanyika jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema kuwa wananchi wamekua wakielekeza malalamiko yao kwa wanataaluma mbalimbali juu ya huduma mbaya, kukiuka maadili ya kitaaluma na kutojaliwa wagonjwa wakiwemo  watoa huduma.

Amesema malalamiko ya wananchi yamekuwa yakitolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, wananchi mmoja mmoja na kupitia mifumo ya kutoa mrejesho ya Wizara ya Afya.

“Tumeshuhudia malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi kwenye vituo vya umma na hata kutoka kwenye hospitali binafsi, nawashukuru pale mlipofuatilia malalamiko hayo maeneo mbalimbali ya nchi yetu ili kubaini makosa na kuchukua hatua stahiki”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri huyo amewasisitiza wenyeviti na wasajili hao kutoa adhabu kali sana kwa wale wachache wanaokaidi miiko na kanuni za maadili yao.

“Msiwaonee aibu, malalamiko haya yanapozidi wananchi watakata tamaa na kuikosa imani kwa Serikali yao ambayo imefanya juhudi kubwa kusogeza huduma za afya kwa wananchi”. Amesisitiza Waziri Ummy.

Amesema viongozi hao wanao wajibu mkubwa wa kusimamia maadili ya wanataaluma ili kuilinda jamii na huduma zinazotolewa kwa wananchi kwa kuhakikisha huduma zinatolewa kwa kiwango kinachofaa na ni salama.

“Serikali chini ya Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu imewekeza katika miundombinu ya afya na kuboresha mazingira ya kutolea huduma pamoja na kutoa ajira kwa watoa huduma za afya kote nchini.

“Kwa msingi  huu mna nafasi kubwa sana ya kuisaidia Wizara ya Afya katika kipaumbele kikubwa mwaka huu yaani kuongeza ubora wa huduma za afya nchini”. Amesisitiza Waziri Ummy.

Ameongeza kuwa wananchi wana haki ya kupata huduma bora, na kuwataka wanataaluma watambue hilo na kutimiza wajibu wao kwa moyo wa upendo bila kusukumwa au kuona wanawatendea hisani wateja wao. 

“Mtoa huduma yeyote awe kwenye vituo binafsi ama ya serikali  ana wajibu huu na wala sio hisani.

“Naagiza mkasimamie hili ili wanataaluma waelewe na wapende kutimiza wajibu huu bila shuruti”.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ametoa wito kwa Wenyeviti na Wasajili wa Mabaraza na Bodi  kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kujikinga na magonjwa mbalimbali.

Previous articleWENYEVITI NA WASAJILI WA MABARAZA SIMAMIENI MAADILI YA WANATAALUMA – WAZIRI UMMY 
Next articleKAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YAPOKEA TAARIFA YA UTENDAJI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here