Home BUSINESS WAFANYAKAZI BENKI YA NMB WASHEREHEKEA MIAKA 59 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA...

WAFANYAKAZI BENKI YA NMB WASHEREHEKEA MIAKA 59 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA KUFANYA USAFI

Katika kusherekea maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar, wafanyakazi wa Benki ya NMB kutoka matawi ya Zanzibar wameungana na Baraza la Udhibiti la Mifumo wa utoaii Leseni (BLRC) Zanzibar kufanya usafi Kwenye viwanja vya Maisara.

Hii ikiwa ni ushiriki wao kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zilizopangwa na serikali katika kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi Zanzibar.

Benki hiyo ni mmoja wa wadhamini wa michuano ya kombe la Mapinduzi yatakayofanyika kesho uwanja wa Amaan.

Wafanyakazi wa Benki ya NMB, Zanzibar pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Udhibiti la Mifumo wa utoaji Leseni (BLRC) wakishiriki kufanya usafi wa viwanja vya Maisara ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Mwaka 1964.

Meneja wa Biashara za Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Shaame (wapili kulia) pamoja na baadhi ya watumishi wa Benki ya NMB na Baraza la Udhibiti wa Mifumo ya utoaji Leseni (BLRC) Zanzibar wakiwa katika shuguli za kuvisafisha viwanja vya maisaraikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 59 ya mapinduzi matakatifu ya Zanzibar.



Previous articleMFUKO WA PAMOJA WA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA OMAN KUANZISHWA
Next articleRAIS  MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI KWA MWAKA 2023 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here