Home LOCAL SUA WAANDAA SERA YA KUDHIBITI UNYANYASAJI WA KINGONO

SUA WAANDAA SERA YA KUDHIBITI UNYANYASAJI WA KINGONO

   Kiongozi wa Masuala ya Jinsia kwenye mradi wa wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET) Prof. John Jeckoniah akieleza malengo ya Kikao kazi hicho cha kupitia Rasimu hiyo.
 

 Mtafiti nguli wa masuala ya Jinsia Prof. Fatihiya Masawe akiwasilisha rasimu hiyo ya sera ya chuo ya masuala ya ukat na unyanyasaji wa kijinsia na muongozo wa utekelezaji wake kabla ya kuanza kujadiliwa.

 Picha ya pamoja ya Baadhi ya washiriki wa kikosi kazi hicho cha kupitia rasimu ya masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na muongozo wa utekelezaji wake.Wajumbe wa kikosi kazi hicho wakifuatilia uwasilishwaji wa Rasimu na kusikia malengo yake.

Kikao kazi hicho kikiendelea.
Wajumbe wa kikosi kazi hicho wakifuatilia uwasilishwaji wa Rasimu na kusikia malengo yake.

Na Calvin Gwabara, Kibaha Pwani.

WATAALAMU na wadau wabobevu wa masuala Jinsia wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha

Kilimo wamekutana kukamilisharasimu ya
Sera ya chuo ya masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na
muongozo wa utekelezaji wake katika kuelekea uanzishwaji wa  kitengo cha jinsia na hatimaye Dawati la
Jinsia.

 Akieleza malengo ya kikao kazi hicho
cha siku mbili Kiongozi wa Masuala ya Jinsia kwenye mradi wa wa Elimu ya juu
kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET) Prof. John Jeckoniah amesema kuwa ni kupitia
rasimu hiyo ya Sera na Muongozo wake ili baadae uweze kuwasilishwa kwa uongozi
wa Chuo kwa kuidhinishwa kupitia kwenye vikao vya maamuzi ya Chuo kupata Baraka
na kuanza kutumika.

“Tumeona tuwakutanishe wataalamu hawa wa masuala ya Jinsia kutokana kuwa na
uzoefu kutoka kwenye taasisi mbalimbali na Idara za Chuo chetu tuweze kuungalia
na kuuboresha vizuri ili uweze kufaa na kutekelezeka kwenye chuo chetu na hivyo
SUA kuwa na mazingira salama kwa kila mmoja anayetoa na kupata huduma wakiwemo
Wahadhiri,Wafanyakazi waendeshaji,Wanafunzi pamoja na watoa huduma wengine
chuoni kwetu” Alieleza Prof. Jeckoniah.

Kiongozi wa masuala ya Jinsia kwenye mradi wa HEET amesema kazi ya
utengenezaji wa rasimu ya  Sera ya
Unyanyasaji na ukatili wa kijinsia (ikiwa ni pamoja na masuala ya ukatili wa
Kingono) na muongozo wa utekelezaji wake ni sehemu ya utekelezaji wa muongozo
wa Wizara Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kutaka kila
Chuo kuwa na dawati la jinsia.

Aidha amesema kuwa kutokana na umuhimuwa wa jambo hilo wamefanikiwa kupata
fedha kupitia mradi wa HEET na hivyo kusaidia kukamilisha kazi hiyo,Ununuzi wa
vifaa kwaajili ya uanzishwaji wa kitengo cha jinsia na dawati la jinsia, kutoa
elimu kwa wanajumuiya kwenye kampasi zote ili masuala hayo yaweze kueleweka
vizuri kwa Chuo kizima na endapo  uongozi
utaipitisha na kuanza kutumika  ili
kuweka na kuwezesha mazingira salama kwa kujifunza na kufanya kazi kwa wadau
wote wa chuo.

Prof. Jeckoniah amewataka wajumbe wa kikosi kazi hicho kushiriki kikamilifu
kutoa mchango chanya na mapendekezo ambayo yatasaidia SUA kupata Sera nzuri
zaidi ambayo itasaidia Chuo kuwa na mazingira salama kwa kila mmoja anapotoa na
kupokea huduma.

Akizungumzia safari toka mwanzo hadi kupatikana kwa rasimu ya sera hiyo na
muongozo wake wa utekelezaji mtafiti na nguli wa masuala ya Jinsia Prof.
Fatihiya Masawe amesema ilichochewa na Mradi mdogo wa maswala ya Unyanyasaji wa
kingono ambao matokeo yake ilikuwa ni kupatikana kwa rasimu hiyo.

Amesema wakati wa uandaaji wa Sera hiyo walitembea kujifunza kwenye vyuo
mbalimbali nchini kama vile Chuo kikuu cha Dar es salaam, Chuo Kikuu cha
Ardhi,DUCE, Chuo Kikuu cha Muhimbili na vyuo vingine  kuona namna wanavyoshughulika na masuala hayo
na kukabiliana nayo.

Prof. Fatihiya amebainisha kuwa pamoja na mambo mengi mazuri waliyojifunza
kwenye maeneo waliyotembelea changamoto kubwa imekuwa ni utayari wa viongozi
katika kutoa rasilimali ili kutekeleza Sera hiyo na hii inatokana na sera
yenyewe kuwa mwiba mchungu kwa wanajumuiya wake wasiofuata maadili bora ya
utendaji kazi kwa kutoa adhabu ambazo zinagusa maisha na ajira za wahusika.

“Ukiona wenye madaraka wanapata kigugumizi kuwepo kwa sera ya masuala hayo
utajua kuwa kweli kuna changamoto lakini sera hii ni kifaa muhimu ambacho pia
kinamsaidia kiongozi kuchukua hatua stahiki dhidi ya watenda makossa hayo na
wanaotendewa na hii itawezekana kama utajengwa uelewa na kuwapa watu nafasi
ya  kutoa taarifa za matendo hayo ili
yakomeshwe” Alieleza Prof. Fatihiya.

Mbobevu huyo wa masuala ya Jinsia amesema Kuwepo kwa Sera hiyo sio tuu
kutasaidia kuweka mazingira bora ya kazi na kujifunzia kwa wote kwenye taasisi
bali kunawezesha kupatikana kwa miradi mbalimbali ya utafiti na maendeleo
kwenye taasisi kwakuwa kuna baadhi ya wafadhili hawakubali kutoa ufadhili
kwenye miradi inayotekelezwa na taasisi ambazo hazina sera ya kudhibiti masuala
ya unyanyasaji na ukatili wa kijinisa ikiwa pamoja na ukatili wa kingono.

Changamoto na matukio ya unyanyasaji wa kingono yamekuwa yakiripotiwa mara
kwa mara kutoka kwenye vyuo mbalimbali na taasisi zingine na uwepo wa Sera na
dawati mahususi kwaajili ya kushughulikia masula hayo kutasaidia kuongeza elimu
na kupunguza matendo hayo na waathirika na kuleta usawa na usalama kwa jamii.

Previous articleRAIS SAMIA:. VYAMA VYA SIASA SASA RUKSA MIKUTANO YA HADHARA
Next articleRAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKITANGAZA KUHUSU KUFANYIKA KWA MIKUTANO YA HADHARA KWA VYAMA VYA SIASA NCHINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here