Home SPORTS SIMBA SC YAIZAMISHA DODOMA JIJI 1-0

SIMBA SC YAIZAMISHA DODOMA JIJI 1-0

Wekundu wa Msimbazi Simba SC imefaniwa kuchukua alama tatu ugenini kwa kuichapa timu ya Dodoma Jiji bao 1-0 katika Dimba la Jamhuri Jijini humo..

Goli la Simba SC lilipachikwa kambani na mshambuliaji wake Baleke Othos J dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Kipindi cha pili timu zote zilirudi uwanjani na nguvu mpya zikicheza kwa kushambuliana lakini hadi mwamuzi wa mchezo huo anapuliza filimbi ya mwisho kumaliza mtanange huo,  timu ya Simba SC ndio waliotoka kifua mbele kwa ushindi wa goli moja.

kufuatia matokeo hayo timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC inaendelea kushikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Ku ya NBC ikiwa na alama 50 ikiwa nyuma ya watani wao wa jadi Young Africans yenye alama 53.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here