Home LOCAL SHESHI LA POLISI GONGO LA MBOTO LAPIGA MARUFIKU VIGODORO KUKESHA 

SHESHI LA POLISI GONGO LA MBOTO LAPIGA MARUFIKU VIGODORO KUKESHA 

Na: Heri Shaaban (Ilala )

JESHI la Polisi Kata ya Gongolamboto limepiga marufuku vingoma vya Mtaani maarufu vigodoro kukesha katika kata ya Gongolamboto kwa ajili ya Usalama wa raia na mali zao.

Jeshi la Polisi limeagiza Wananchi wote wenye shughuli za vigodoro waanze s
asubuhi mpaka Jioni wawe wamemaliza Shughuli watakao kaidi agizo watachukuliwa hatua na Jeshi la Polisi.

Akizungumza katika mkutano wa Serikali za Mtaa Ulongoni Gongolamboto ulioandaliwa na Mwenyekiti Abdulrahim Munisi OCD wa Gongolamboto A/ISP Charles Kishai alisema katika kata hiyo Shughuli za vigodoro zinatakiwa kuanza asubuhi mpaka jioni na shughuli za ukumbini mwisho saa sita usiku .

OCD Charles alisema wananchi wengi wameweka utaratibu wa kukesha na vigodoro mitaani jeshi la polisi litawakamata wote watakaovunja Sheria na taratibu .

“Tunawaomba Wananchi wote wenye shughuli kufuata utaratibu Serikali za Mitaa ili uweze kupewa kibali “alisema OCD Charles.

Akizungumzia Ulinzi na Usalama amewataka apewe Ushirikiano katika masuala ya Ulinzi Ikiwemo kupewa taarifa za siri bila kusingiziana kesi .

Aliwataka Wananchi wa Ulongoni kutoa taarifa za uharifu ikiwemo kutunza Siri za uharifu sambamba na kulipa tozo ya Ulinzi Shirikishi .

Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Ulongoni Kata Gongolamboto Abdulrahim Munisi aliwataka wananchi watoe tozo kwani ukitoa tozo sawa umelinda

Mwenyekiti Munisi alisema suala la Ulinzi shirikishi lipo kisheria amewataka Wananchi walipe tozo ya Ulinzi kukwepa kifungo .

Aidha alisema Mwananchi ukikamatwa ujatoa tozo ya Ulinzi sawa na muharifu hivyo utachukuliwa hatua za kisheria .

Mwisho

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 9-2023
Next articleMIZUNGU AWATAKA VIJANA ILALA KUSIMAMA KIDETE KATIKA MIRADI YA CHAMA 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here