Home LOCAL SERIKALI YAJIPANGA KUIBORESHA HOSPITALI YA MIREMBE

SERIKALI YAJIPANGA KUIBORESHA HOSPITALI YA MIREMBE

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imefanya maboresho ya miundombinu yaliyogharimu zaidi ya Bilioni 6 katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili-Mirembe

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ujenzi na kuongea na watumishi wa hospitali hiyo Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema ujenzi huo umefikia hatua za mwisho hivyo itasaidia wananchi kupata huduma za afya katika mazingira bora

“Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya Bilioni 6 katika kuboresha miundombinu pamoja na vifaa tiba katika hospitali hii, sasa ni jukumu lenu watumishi kuboresha na kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo matumizi ya lugha nzuri”Alisisitiza Dkt. Mollel

Aidha, Dkt. Mollel ameiagiza MSD ndani ya miezi miwili kuhakikisha inapeleka vifaa vya upasuaji wa mifupa katika hospitali hiyo ili wananchi waanze kunufaika na huduma hiyo ambayo awali walikua wakiifuata umbali mrefu.

“MSD leteni vifaa vya upasuaji dani ya miezi miwili pia mnatakiwa kutoa kibali cha kununua dawa kwa watu binafsi kwa vituo vyote vya kutolea hhuduma za afya nchini ndani ya saa 24 endapo dawa zinahitajika na hazipo MSD ili kuondoa usumbufu unaoweza kuzuilika kwa wananchi”Alisisitiza

Hata hivyo Dkt. Mollel amewashauri viongozi wa hospitali hiyo kuanza kufikiria namna ya kuongeza huduma nyingine ili kutanunua wigo wa kuwahudumia wananchi wenye uhitaji bila kuathiri huduma maalumu za magonjwa ya afya ya Akili zinazotolewa katika Taasisi hiyo.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri huyo ameagiza hospitali hiyo kupatiwa gari ya kubebea wagonjwa kutokana na unyeti wa huduma katika hospitali hiyo ili kuokoa maisha ya wananchi wanaohitaji huduma hiyo.

Vile vile Dkt. Mollel amewaelekeza Wakuu wa Hospitali zote nchini kuacha tabia ya kuwazuia wagonjwa wa rufaa kutoka kituo kingine chochote bila kujali huduma ya mgonjwa huyo ni wa msamaha au la,hiyo itasaidia kuondoa changamoto kwa wagonjwa ikiwemo vifo vinavyoweza kuzuilika.

Naye,Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Afya Bi. Deodatha Makani amesema wakati hospitali hiyo inaelekea kuwa taasisi ni muhimu watumishi kujipanga na kuwahuduma wananchi kwa ubora wa juu ili kuendana na hadhi ya kuwa taasisi, huku akiweka wazi kwamba Wizara itaendelea kutatua changamoto zote za watumishi.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Wizara ya Afya Prof. Paschal Ruggajo amesema wakati Serikali inaelekea kutekeleza Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote lazima viongozi na watumishi wajipange vizuri katika utendaji wao ikiwemo kuboresha na kutoa huduma bora kwa wananchi hasa matumizi ya lugha nzuri na muda mfupi wa kuwahudumia wananchi wanaofika kupata huduma

Mwisho.

Previous articleBENKI YA CRDB YAONESHA NJIA MFUMO WAMALIPO KIDIJITALI WA BANDALI
Next articleSUALA LA UPANDAJI MITI LINAPASWA KUWA LA LAZIMA – MAKAMU WA RAIS DKT MPANG
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here