Home LOCAL SEKTA YA KILIMO KUKUA KWA 10% IFIKAPO 2030 – RAIS SAMIA

SEKTA YA KILIMO KUKUA KWA 10% IFIKAPO 2030 – RAIS SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kansela wa Ujerumani Mhe. Olaf Scholz, Davos nchini Uswizi tarehe 18 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kansela wa Ujerumani Mhe. Olaf Scholz mara baada ya mazungumzo yao Davos nchini Uswizi tarehe 18 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Kansela wa Ujerumani Mhe. Olaf Scholz mara baada ya mazungumzo yao Davos nchini Uswizi tarehe 18 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji ambaye pia ni Mwazilishi wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) Profesa Klaus Schwab Mjini Davos nchini Uswizi tarehe 18 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji ambaye pia ni Mwazilishi wa Jukwaa la Uchumi Duniani Profesa Klaus Schwab mara baada ya mazungumzo Mjini Davos nchini Uswizi tarehe 18 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Poland Mhe. Andrzej Duda mara baada ya mazungumzo Davos nchini Uswizi tarehe 18 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Poland Mhe. Andrzej Duda mara baada ya mazungumzo Davos nchini Uswizi tarehe 18 Januari, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema sekta ya kilimo nchini inatarajiwa kukua kwa 10% ifikapo mwaka 2030 ukilinganisha na ukuaji wa sasa wa takriban 3.6%.  

Rais Samia amesema Tanzania imetengeneza fursa za kitaifa kwa ajili ya mabadiliko ya mfumo wa chakula unaotarajia kuongeza uzalishaji wa chakula, kuimarisha maisha ya watu na kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. 

Akichangia kwenye mada inayohusu masuala ya chakula ‘Food Action Partnership: Investing in Greater Resilience’, ikiwa mkutano mwingine wakati wa Jukwaa la Uchumi Duniani, Uswizi Rais Samia alizungumzia dira ya mabadiliko ya kilimo Tanzania. 

Katika kudhibiti mfumo endelevu wa chakula nchini, Rais Samia amesema jitihada kadhaa zimefanyika, ikiwemo kuanzisha mradi kwa ajili ya vijana huku wakiendelea kuimarisha ukuaji wa shoroba za kilimo. 

Jitihada nyingine zilizofanyika kuanzia mwaka huu wa fedha ni pamoja na kuongeza bajeti ya kilimo mara 4 ukilinganisha na ile iliyopita. Aidha, Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika mwezi Septemba kudhihirisha maendeleo hayo.  

Mdahalo huo ulihudhuriwa na zaidi ya Viongozi 50 kutoka Afrika, Asia, Ulaya na Marekani kwa nia ya kuongeza kasi ya ushirikiano na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya kila nchi. 

Wachangiaji wakuu katika mdahalo huo mbali na Rais Samia walikuwa Rais Gustavo Petro wa Colombia, Tran Hong Ha, Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam na Bw Alvaro Lario, Rais wa Wakfu wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Roma.

Previous articleTAASISI ZINAZOENDELEA NA UJENZI WA OFISI ZATAKIWA KUKAMILISHA MAJENGO YAO KWA WAKATI JIJINI DODOMA
Next articleTANZANIA NA CHINA ZASAINI MUHTASARI WA TAARIFA YA UPEMBUZI YAKINIFU YA UJENZI NA UPANUZI WA JKCI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here