Home BUSINESS RAIS SAMIA AWAPONGEZA VIJANA WA KITANZANIA KWA KUPATA MEDALI YA FEDHA

RAIS SAMIA AWAPONGEZA VIJANA WA KITANZANIA KWA KUPATA MEDALI YA FEDHA

*Ni baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya ubunifu duniani

MHESHIMIWA Rais Dkt. Samia Suluhu Hssan amewapongeza vijana wa Kitanzania walioibuka washindi wa pili na kupata medali ya fedha katika mashindano ya kwanza ya Global Robotics Challenge yaliyofanyika Geneva Uswisi na kushirikisha mataifa zaidi ya 190.

Amefarijika kusikia kuwa roboti iliyoundwa na vijana kutoka Tanzania chini ya maudhui ya kukamata hewa ukaa (Carbon dioxide) inaweza kusaidia kusafisha kaboni hewani na kusaidia kupunguza ongezeko la joto kwenye angahewa ya Dunia.

Kauli hiyo imetolewa leo (Jumapili, Januari 15, 2023) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia katika hafla ya kuwapongeza vijana hao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

“Nitumie nafasi hii kuwaahidi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari itaendelea kufuatilia maendeleo yenu na kuona namna ya kuendeleza vipaji vyenu.”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuielekeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iandae mpango wa kuwa na vituo vya ubunifu nchini katika ngazi za Mikoa na Wilaya mbalimbali ili kusaidia kuinua vipaji vya vijana.

Amesema Wizara iimarishe utaratibu wa kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu mbalimbali ili kuwamotisha na kukuza ajira nchini na ishirikiane na mamlaka husika kuandaa utaratibu wa kuwasaidia wabunifu mbalimbali na kuwaunganisha na taasisi pamoja na makampuni kwa ajili ya kuendeleza bunifu za kazi zao kulingana na mahitaji.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameipongeza Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kwa kuamua kutumia sehemu ya mapato yao kwa kuwasaidia vijana wa kike nchini katika kuendeleza bunifu nchini kupitia APPS and Girls.

Waziri huyo mesema kuwa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa ushiriki wa mabinti na wanawake katika matumizi ya TEHAMA si mzuri sana, Barani Afrika asilimia 24 tu ya wanawake wanashiriki kwenye TEHAMA huku wanaume ni asilimia 35.

Previous article“HAKIKINI NAMBA KUEPUSHA UHALIFU” – NAIBU WAZIRI KUNDO 
Next articleMWENYEKITI MTEMVU ATOA ONYO WALIOANZA KAMPENI ZA UBUNGE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here