Home LOCAL RAIS SAMIA ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA KUTOA MSAADA KWA VITUO...

RAIS SAMIA ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA KUTOA MSAADA KWA VITUO SABA VYA WATOTO 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa leo tarehe 27 Januari, 2023, Kwa kutoa vitu mbalimbali katika vituo Saba (7) vya Watoto Yatima.

Vitu hivyo Saba vimekabidhiwa mapema leo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mbunge wa Mkuranga Mhe Abdallah Ulega ambaye alimwakilisha Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo aliweza kukabidhi vitu mbalimbali na fedha taslimu

Tukio hilo limefanyika katika Kituo Cha Children home Msimbazi cha Ilala Jijini Dar es Salaam.

Ulega pia aliweza kukabidhi zawadi hizo kwa Kituo cha Watoto Mburahati.

Katika tukio hilo, pia aliweza kutembelea na kujulia hali watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho cha Msimbazi.

Vitu vilivyokabidhiwa ni pamoja na pempasi za watoto, unga, Sabuni, sukari, maziwa, mafuta na vingine vingi.

Aidha, vituo vingine ambavyo vimepelekewa zawadi hizo ni pamoja na Vituo vya Tuangoma, Mbagala, Mbweni, Mwasonga na Sinza

Mwisho.

Previous articleTANZANIA, INDIA KUFUNGUA FURSA MPYA ZA BIASHARA
Next articleBENKI YA CRDB YAKABIDHI MADARASA MAWILI SHULE YA MSINGI CHUDA, JIJINI TANGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here