Home SPORTS JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA SONGEA DKT YOSE MLYAMBINA AFUNGA...

JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA SONGEA DKT YOSE MLYAMBINA AFUNGA BONANZA LA WIKI YA SHERIA,AITAKA JAMII KUPENDA KUSHIRIKI MICHEZO ILI KULINDA AFYA NA KUDUMISHA MAHUSIANO

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea Dkt Yose Mlyambina akikagua timu mbalimbali za mpira wa miguu ya kabla ya kufunga Bonanza la michezo mbalimbali katika uwanja wa shule ya msingi Sokoine Manispaa ya Songea,

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea Dkt Yose  Mlyambina akizungumza kabla ya kufunga bonanza la michezo katika uwanja wa shule ya msingi Sokoine Manispaa ya Songea,kulia kwake Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Songea Upendo Madeha.

Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea DDkt Yose Mlyambina katikati, Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Songea Upendo Madeha wa tatu kushoto, wakiwa katika picha ya pamoja na wadau waliofanikisha bonanza la michezo mbalimbali lililoandaliwa na mahakama  katika wiki ya sheria nchini.

Na: Mwandi Maalum, Songea

JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuuu kanda ya Songea Dkt Yose Mlyambina,amewaongoza watumishi wa mahakama,taasisi na idara za serikali katika bonanza la michezo mbalimbali likiwa na lengo la kuboresha afya ,kujikinga na magonjwa,kuleta mahusiano na kufahamiana.

Akizungumza kabla ya kufunga Bonanza hilo lililofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Sokoine Manispaa ya Songea Jaji  Dkt Mlyambina,amewahimiza vijana mkoani Ruvuma kutumia muda wao kufanya mazoezi na kushiriki katika michezo mbalimbali ili kujiweka sawa kiafya,kiakili badala ya kutumia muda wao kwenye ulevi.

Alisema,bonanza hilo limekuwa na faida nyingi ikiwamo kuboresha afya, kuimarisha mahusiano kati ya watumishi  na wadau wa mahakama na taasisi  nyingine za serikali,kufahamiana na kuondoa ukuta(wigo)kati ya mahakama na wananchi.

Alisema,mtu anayefanya mazoezi kwa kawaida anakuwa na afya ya akili,ana imarisha mwili na kuongeza siku  za kuishi na kuwaasa wananchi wa mkoa huo ,kuwa na utaratibu wa kushiriki katika michezo na mabonza mbalimbali ili kulinda afya zao.

Aidha Jaji Dkt Mlyambina alisema,katika maadhimisho ya wiki ya sheria watumishi wa mahakama wametoa elimu ya sheria kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,sokoni,na wananchi waliofika kwenye mabanda ya maonyesho katika viwanja vya soko kuu Songea.

Bonanza la Wiki ya Sheria  lilifunguliwa tarehe 23 mwezi huu na limefungwa jana tarehe 29 Januari chini  ya‘Kauli mbiu umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu na wajibu wa mahakama na wadau’.

Kwa upande wake mdau wa michezo meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Ephatar Mlavi,ameipongeza mahakama kanda ya Songea kuandaa bonanza  hilo kwani limesaidia kukutanisha wadau mbalimbali,watumishi wa idara  na taasisi za serikali na wananchi.

Alisema,bonanza hilo limekuwa na mafanikio makubwa kwani limewezesha  washiriki kupata nafasi ya kufanya mazoezi na kuboresha afya zao na kushauri liendelee kufanyika mwaka hadi mwaka.

Awali mratibu wa bonanza hilo wakili Abel Ngilangwa,alitaja michezo iliyochezwa ni mpira wa miguu kwa wanaume,mpira wa pete,kufukuza kuku,kukimbia kwenye magunia mbio za mita 100 na 200,kuvuta kamba,kukimbia na yai kwenye kijiko na kukimbiza kuku.

Ngilangwa alieleza kuwa,lengo kuu la bonanza hilo ni kutoa elimu ya sheria,kuimarisha mahusiano kati ya Mahakama na wananchi,kuimarisha afya za watumishi kupitia michezo ili kuondoa magonjwa yasiyoambukiza.

Alisema,michezo hiyo ni kielelezo halisi kinacho thibitisha jamii umoja na ushirikiano ndani ya mahakama katika kuhakikisha lengo la mahakama kuu Tanzania kuifikia jamii na ni chombo kinachofikika kwa urahisi.
MWISHO.

Previous articleSERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 1.4 KUJENGA SHULE TATU ZA SEKONDARI WILAYANI TUNDURU,WAZAZI WAIPONGEZA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU
Next articleCCM HAITAACHA KUHOJI WATENDAJI WA SERIKALI – CHONGOLO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here