Home BUSINESS GAVANA EMMANUEL TUTUBA APOKELEWA NA PROFESA FLORENS LUOGA BoT

GAVANA EMMANUEL TUTUBA APOKELEWA NA PROFESA FLORENS LUOGA BoT

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT  Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba akilakiwa na Gavana wa Benki Kuu hiyo aliyemaliza muda wake Prof Florens Luoga mara baada ya kwasili Makao Makuu ya benki hiyo Jana Januari 9, 2023 jijini Dodoma, Bw. Emmanuel Tutuba alikula kiapo Cha Maadili ya Utumishi wa Umma Jana Ikulu Chamwino mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba, amelakiwa na Gavana Mstaafu, Prof. Florens Luoga alipowasili kwa mara ya kwanza Makao Makuu ya BoT jijiji Dodoma Januari 9, 2023 ikiwa ni saa chache baada ya Kula kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma IKULU, Chamwino.

Wengine waliomlaki Gavana Tutuba ni Manaibu Gavana pamoja na wafanyakazi wa BoT.

Gavana Emmanuel Mpawe Tutuba anakuwa Gavana wa Nane wa Benki Kuu ya Tanzania yangu nchi yetu ipate Uhuru 1961.

Gavana wa kwanza alikuwa Bw. Edwin Mtei aliyeongoza Benki Kuu kuanzia Juni 1966 hadi Januari 1974.

Alifuatiwa na Bw. Charles Nyirabu aliyehudumu kuanzia Januari 1974 hadi Januari 1989. Gavana aliyefuatia ni Bw. Gilman Rutihinda kuanzia Januari 1989 hadi Januari 1993. 

Gavana Rutihinda alirithiwa na Dkt. Idris Rashid kuanzia Januari 1993 hadi Januari 1998. Kuanzia Januari 1998 Benki Kuu ya Tanzania iliongozwa na Dkt. Daudi Ballali hadi Januari 2008 na kufuatia na Profesa Benno Ndulu aliyeongoza kuanzia Januari 2008 hadi Januari 2018.

Kuanzia mwaka 2018 Benki Kuu ya Tanzania iliongozwa na Profesa Florens Luoga ambaye amehudumu hadi Januari 2023.

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 10 – 2023
Next articleMAKAMU WA RAIS AFUNGUA SKULI YA KWALE PEMBA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here