Home LOCAL BALOZI FATMA ATETA NA BALOZI WA ALGERIA

BALOZI FATMA ATETA NA BALOZI WA ALGERIA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Algeria nchini, Mhe. Ahmed Djellal katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Januari 2023.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao walijadili kuhusu masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Algeria kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Kwa upande wake Balozi wa Algeria nchini, Mhe. Ahmed Djellal aliongea kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Algeria na Tanzania hususani diplomasia ya kimataifa, kukuza na kuimarisha biashara, uwekezaji na utalii baina ya nchi zetu mbili.

“katika mazungumzo yetu leo, tumekubaliana kuendelea kuimarisha diplomasia baina ya mataifa yetu kwa maslahi mapana ya nchi zetu na kwa maendeleo ya wananchi wetu,” amesema Balozi Djellal .

Balozi Fatma amesema kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Algeria katika sekta mbalimbali kama vile za nishati, elimu, afya na miundombinu kwa maendeleo ya mataifa yote mawili.

Algeria ilifungua Ubalozi wake nchini Tanzania mwaka 1964 ikiwa ni miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa kufungua ubalozi hapa nchini. Mwaka 1981 nchi hizi mbili zilianzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) ambayo imechangia kuimarisha na kukuza ushirikiano wake na Tanzania.

Previous articleRAIS DKT.HUSSEIN MWINYI AFUNGUA DIKO NA SOKO LA SAMAKI MALINDI UNGUJA
Next articleMIRADI 215 YASAJILIWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI ZANZIBAR- MAJALIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here