Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akikata utepe kufungua Kituo cha Maarifa cha Horticulture kinachohudumia kilimo cha mboga mboga,viungo na matunda kiliopo Mpendae, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi,hafla iliyofanyika leo ambapo viongozi mbali mbali walihudhuria leo.[Picha na Ikulu] 31/01/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Viongozi wa Taasisi ya TAHA (kulia) Bi.Jacqueline Mkindi Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TAHA Mhandisi Zebadiah Moshi,wakati alipofika katika ufunguzi wa Kituo cha Maarifa cha Horticulture kinachohudumia kilimo cha mboga mboga,viungo na matunda kiliopo Mpendae, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi leo.[Picha na Ikulu] 31/01/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akipokea zawadi ya Ndizi Ali Hassan Mwinyi kutoka kwa Ndg.Zulpher Viungo katika Mradi wa Viungo unaosimamiwa na Agriconect Mwanakwerekwe leo wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya bidhaa za kilimo katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Maarifa cha Horticulture kinachohudumia kilimo cha mboga mboga,viungo na matunda,Mpendae Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi .[Picha na Ikulu] 31/01/2023.
Baadhi ya Wananchi na wafanyakazi wa TAHA wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika sherehe za Ufunguzi wa Kituo cha Maarifa cha Horticulture, kinachohudumia kilimo cha mboga mboga,viungo na matunda,kilichopo Mpendae Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi .[ Picha na Ikulu] 31/01/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya TAHA Ndg.Amani Temu (wa pili kulia) alipokuwa akitoa maelezo jinsi wanavyotoa huduma wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya bidhaa za kilimo katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Maarifa cha Horticulture kinachohudumia kilimo cha mboga mboga,viungo na matunda leo ,Mpendae Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi .[Picha na Ikulu] 31/01/2023.