Home SPORTS YANGA YAENDELEZA UBABE WA USHINDI, YAICHAPA COASTAL UNION 3-0 KWA MKAPA

YANGA YAENDELEZA UBABE WA USHINDI, YAICHAPA COASTAL UNION 3-0 KWA MKAPA

Timu ya wananchi Yanga SC imeibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-0 kwa kuizamisha timu ya Coastal Union ya Tanga kwenye mchezo uliopigwa katika Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Magoli ya wababe hao wa Jangwani yamepachikwa kambani na mshambuliaji wa kimataifa raia wa Congo Fiston Mayele aliyepachika mabao 2 katika dakika ya 28 na 47 kipindi cha kwanza muda mfupi kabla ya kwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Yanga wakionekana kuwa imara zaidi kwa kulishambulia lango la wagosi wa kaya Costal Union walioonekana kuzidiwa katika maeneo yote.

Feisal Salum ‘Feitoto’ alishindilia msumari wa 3 katika dakika ya 67 ya mchezo huo kwa shuti kali akimalizia mpira uliotengwa na Steven Azizi Ki aliyekuwa katika kiwango kizuri katika mchezo huo.

Kutokana na matokeo hayo Yanga imeendelea kubaki kileleni cha msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu Simba SC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here