Home SPORTS YANGA SC YAENDELEA KUONGOZA LIGI KUU YA NBC IKIICHAPA AZAM 3-2 KWA...

YANGA SC YAENDELEA KUONGOZA LIGI KUU YA NBC IKIICHAPA AZAM 3-2 KWA MKAPA

Ni mtanange wa kuktata na shoka ukiwakutanisha wababe wa soka Matajiri wa Jiji la Dar es Salaam kutoka Chamazi timu ya AZAM FC na Young Africans ya Jangwani Kariakoo ya Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Ligi kuu soka ya NBC Tanzania bara umepigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 bao la kwanza likifungwa katika dakika ya 27 na mshambuliaji wake Hamisi Suleiman Sopu akiunganisha krosi safi ya Price Dube.

Iliwachukuwa dakika 4 tu baadaye Yanga kusawazisha bao hilo likipachikwa kambani na Mshambuliaji wa kimataifa raia wa Congo Fiston Mayele katika dakika ya 30 ya mchezo huo, na dakika 2 tu baadaye Stephae Azizi ki alipachika bao la pili dakika ya 32 kwa shuti kali llilomshinda mlinda mlango wa AZAM FC Ahmes Ahmada goli lililodumu katika kipindi chote cha kwanza cha mchezo huo.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa kila timu kulisakama lango la mwenzake ambapo timu ya AZAM kusawazisha kwa kupachika bao la pili lililowekwa kambani na Hamisi Suleiman SopuĀ  katika dakika ya 46 ya kipindi cha pili na kumfanya mshambuliaji huyo kutupia mabao mawili peke yake katika mchezo huo.

Timu ya Yanga ilipachika msumari wa tatu mnamo dakika ya 77 ya kipindi cha pili likifungwa na Farid Mussa Mariki akiunganisha mpira uliotemwa na Mlinda mlango wa AZAM FC Ali Ahmada kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Stephane Azizi Ki.

Previous articleRIDHIWANI KIKWETE ATOA AGIZO FEBRUARY KIVULE WAPATE HATI WOTE
Next articleMAGAZETI YA LEO DISEMBA JUMATATU 26,2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here