Home BUSINESS WAZIRI MBARAWA AITAKA MAMLAKA YA BANDARI NCHINI KUTANGAZA MABORESHO MAKUBWA YALIYOFANYIKA BANDARI...

WAZIRI MBARAWA AITAKA MAMLAKA YA BANDARI NCHINI KUTANGAZA MABORESHO MAKUBWA YALIYOFANYIKA BANDARI YA MTWARA

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amewata Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) kutangaza maboresho makubwa ambayo yamefanyika katika bandari ya Mtwara ili iweze kutumika ipasavyo.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha Bandari ya Mtwara inaendelezwa na kuwa kituo kikubwa cha usafirishaji katika ukanda wa kusini na nchi za jirani.

Makame ametoa mwito huo leo wakati alipotemebelea bandari ya Mtwara kuangalia utendaji kazi katika bandari hiyo.

“Watu wa TPA haya mambo mazuri nendeni mkayatangaze , mkawaambie wafanyabiashara kwamba bandari ya Mtwara sasa imefunguka ,gharama za usafirishaji zimepungua Kwa asilimia kubwa,” amesema.

Mbarawa amesema TPA wakitangaza bandari ya Mtwara ndani ya nje ya Tanzania wafanyabiashara wengi watakuja na kuhakikisha bandari hiyo inafanya kazi usiku na mchana.

Baadhi ya gharama zilizopunguzwa ni za gharama za kusafirisha mizigo kwenye meli (wharfage charges) kwa nusu gharama ikilinganishwa na baadhi ya bandari hapa nchini, gharama za kupakia na kupakua mizigo kutoka kwenye meli kwenda kwenye gati Kwa asilimia 70.

Pia katika bandari ya Mtwara, serikali imeongeza siku za mzigo kukaa bandarini.

Serikali pia imeweka vifaa vyote muhimu vya kuwezesha usafirishaji ikiwemo kifaa Maalumu cha kupakua na kupakulia makontana  (Ship to Shore Container Crane)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here