Home Uncategorized WABUNIFU KUTAMBIANA JUKWAA LA RUNWAY BAY ZANZIBAR

WABUNIFU KUTAMBIANA JUKWAA LA RUNWAY BAY ZANZIBAR

Na:  JEREMIA ERNEST

WABUNIFU 12 wanatarajiwa kushiriki kuonyesha kazi zao katika jukwaa la mitindo Runway bay ambalo litafanyika kwa siku tatu.

Huu ni msimu wa tatu tangu kuanzishwa kwa jukwaa hili ambalo limebeba dhima ya kutangaza utalii wa ndani ya visiwa vya Zanzibar.

Akizungumza na ukurasa huu mwandaaji wa jukwaa hilo Waiz Shelukindo, amesema mpaka sasa wabunifu zaidi ya 12 wamesha jisajili kuonyesha ubunifu wao.

“Maandalizi ya jukwaa hili yanafikia ukingoni kuna mambo mengi ambayo tumeboresha msimu huu tuna wabunifu 12, kutoka ndani na nje ya Tanzania kila mmoja amepajipanga kuonyesha tambo zake kumzidi mwenzie,”Anasema Waiz.

Aliongeza kuwa tamasha hilo litafanyika pembezoni mwa barabara ya Mizingani mbali ya maonyesho ya nguo kutakuwa na burudani na utoaji wa tuzo kwa wadau mbalimbali wa tasnia ya mitindo.

Miongoni mwa wabunifu watakao onyesha mavazi yao no Ant Laa, C&G kutoka Zanzibar, Zado fashion Kilimanjaro, Jonjo designer Uganda, Lizzie designer na Peric designer.

Previous articleCHUO CHA BAHARI (DMI) CHAOMBA MIUNDOMBINU YAKE IKARABATIWE
Next articleFORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here