Home SPORTS SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA KAGERA SUGAR KAITABA

SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA KAGERA SUGAR KAITABA

Timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC imelazimishwa sare ya goli 1-1 na timu ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara katika Dimba la Kaitaba Mkoani Kagera.

Timu ya Kagera Sugar ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza kupitia mchezaji wake Deus Bukenya dakika 15 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo akiunganisha mpira wa Kona.

Katika Dakika ya 39 ya mchezo huo Simba walisawazisha goli hilo likifungwa na mlinzi wa kati wa timu hiyo akipiga kichwa Kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Clatus Chama.

Kipindi cha pili timu zote zilionekana kushambuliana huku Kagera wakiimarisha safu yao ya ulinzi kwa kucheza kwa umakini mkubwa huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.

Kufuatia matokeo hayo timu ya Simba SC imeendelea kubaki katika nafasi ya pili ya mchezo huo ikiwa na alama 38 ikiwa chini ya ya mpinzani wake Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania yenye alama 44.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here