Home Uncategorized SERIKALI YAUPONGEZA MRADI WA HPSS KWA MCHANGO WAKE KATIKA UTEKELEZAJI CHF ILIYOBORESHWA

SERIKALI YAUPONGEZA MRADI WA HPSS KWA MCHANGO WAKE KATIKA UTEKELEZAJI CHF ILIYOBORESHWA

Na: Farida Mangube, Morogoro.

 Katika kipindi cha miaka minne Mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa ( iCHF) umekusanya zaidi ya Sh. 30 bilioni kutokana na michango ya wanachama wake na kati ya fedha hizo zaidi ya Sh. 20 bilioni zimerejeshwa katika vituo vya kutolea huduma za afya kama malipo ya gharama za kuhudumia wanachama.

Hayo yamesemwa mjini Morogoro na Mratibu wa mfuko  wa iCHF  kutoka Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Tamisemi Silvery Maganza  kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa wa iCHF ngazi ya mikoa ambao ni wahasibu na maafisa Tehema kuhusu mfumo wa ulipaji Serikalini (MUSE) 

Maganza alisema kuwa kwa sasa mfuko huo una zaidi ya ya wanachama 4 milioni sawa na asilimia 7.6 huku lengo ni kufikia asilimia 80 ya Watanzania walio kwenye sekta zisizokuwa rasmi ambao mara nyingi wamekuwa wakipata changamoto ya matibabu kutokana na kukosa fedha wanapougua.

Akijubu hoja ya idadi ndogo ya wanachama walioandikishwa Maganza alisema kuwa ni kutokana na elimu ndogo kwa wananchi kuhusu mfuko huo na umuhimu wake hivyo amewataka wananchi kujiunga na mfuko huo ili wawe na uhakika wa matibabu.

“wananchi wanatakiwa kujua kwamba ugonjwa unakuja bila ya taarifa , hivyo kuna umuhimu wa kuchangia malipo hayo ya iCHF ili ikitokea mtu ameugua ili aweze kupata huduma ya matibabu”  alisema Maganza.

Hata hivyo alisema mfumo wa tehema unaotumiwa na mfuko huo kwa sasa umeonyesha mafanikiwa makubwa kwa kurahisisha kazi ambapo mwananci anaweza kujiandikisha  na kupata huduma popote nchini

Naye mchambuzi wa maswala ya TEHEMA katika Mradi wa HPSS Tuimarishe afya unaofadhiliwa na Serikali ya Uswis kupitia shirika la Swiss Tropical and Public Heath Institute Nicholas Kanisa alisema kuwa  wao kama wadau kwa kushirikiana na Serikali wamekuwa  wakisaidia maswala mbalimbali yakiwemo ya kiufundi na kifedha ili kuhakikisha kwamba mifumo yote inaunganika kwa kutoa mfunzo ya kuwajengea uwezo .

Kwa upande wake mratibu wa iCHF Mkoa wa Morogoro Elisia Mtesigwa alikili kuwepo kwa  changamoto ya upatikanaji wa dawa hata hivyo alisema kuwa ipo miongozo inayoeleza namna ya utoaji wa huduma za iCHF kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya rufaa ya mkoa

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Mradi wa Tuimarishe afya unaofadhiliwa na Serikali ya Uswis kupitia shirika la Swiss Tropical and Public Heath Institut

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here