Home Uncategorized SERIKALI INAJIANDAA KUWASILISHA BUNGENI MABADILIKO SHERIA YA HABARI – MSIGWA

SERIKALI INAJIANDAA KUWASILISHA BUNGENI MABADILIKO SHERIA YA HABARI – MSIGWA

GERSON Msigwa, Msemaji wa Serikali amesema, serikali inajiandaa kuwasilisha bungeni mabadiliko ya vipengele vya Sheria ya Habari ili wabunge wakiridhia, utekelezaji wake ufanyike.

Alitoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC), uliofanyika katika Ukumbi wa Kisenga.

Alisema, anatambua kuwa katika tasnia ya habari kuna changamoto na miongoni mwayo ni kuhusu sheria zinazohitaji kurekebishwa.

“Kwa sasa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inajiandaa kuwasilisha bungeni mabadiliko ya sheria hii ili wabunge wakiridhia, tuendelee na utekelezaji wake,” alisema Msigwa.

Msemaji huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) alisema, mchakato wa kukutana na wadau kwa ajili ya majadiliano ya vipengele vya sheria hiyo ya mweaka 2016, umekamilika.

“Niwahakikishie kuwa, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ni kutengeneza mazingira wezeshi kwa vyombo vya habari kufanya kazi bila bughudha yoyote.

“Tayari Mheshimiwa Rais ameshamuagiza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kukutana na wadau wa sekta ya habari na kujadili namna ya kuziboresha sheria ambazo siyo rafiki kwa tasnia ya habari,” alisema.

Alisema, miongoni mwa sheria hizo ni ile ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016, ambapo tayari vikao kadhaa kati ya serikali na wadau vimefanyika.

Alisema, serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wa habari nchini katika kukabili changamoto zilizopo.

“Niwahakikishie kuwa, serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wa habari katika kuhakikisha changamoto zote zinazowakabili waandishi wa habari zikiwamo kutatua sheria zisizo rafiki, zinafanyiwa kazi na kuwa na sheria zinazotokana na pande mbili kukubaliana yaani serikali na wadau,” alisema Msigwa.

Previous articleWADAU WA VIWANDA WAVUTIWA NA KAZI ZA TIRDO KATIKA MAONESHO YA BIDHAA ZA VIWANDA DSM
Next articleTCRA YAKUTANA NA WADAU WA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA, YATOA UFAFANUZI HOJA ZA WADAU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here