Na HERI SHAABAN
MKUU wa Mkoa Dar es Salaam Amos Makala amezuia WATENDAJI wa Halmashauri ya Temeke kusafiri mpaka wakamilishe ujenzi wa vyumba vya madarasa Desemba 30 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa Amos Makala,alitoa agizo hilo Wilayani Temeke leo wakati wa Ziara yake endelevu kuangalia ujenzi huo katika mkoa wa Dar es Salaam .
“Natoa agizo akuna kusafiri kwa sasa mpaka mkamilishe ujenzi wa vyumba vya madarasa 207 Desemba 30 Madarasa yawe yamekamilika ambayo yanatakiwa kujengwa katika Wilaya yenu “alisema Makala .
Alisema kazi ya watendaji kusimamia maelekezo ya Rais uongozi ni kazi hivyo wasimamie na kutekekeza katika kumsaidia ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Alisema ziara hiyo imekagua ujenzi wa madarasa Chamazi na Dovya Wilayani Temeke Chamazi inabadirika kila Siku maendeleo ya nchi yetu yanaonekana Rais Samia Suluhu Hassan ametatua kero ya Madarasa na kushukuru ndio Mira ya desturi ya nchi yetu .
Amewataka viongozi wa chama cha Mapinduzi watekekezaji wa Ilani wakishirikiana na Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa wasimamie maeneo ya wazi ,maeneo ya umma ,ni muhimu kuyalinda .
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ng’wilabuzu Ludigija alisema Wilaya ya Temeke wamepokea Shilingi Bilioni 4.1 madarasa 207 yanajengwa changamoto ya maeneo wamefanya upembuzi na uwamuzi shule mbili za gholofa zinajengwa .
Ludigija alisema ujenzi unaendelea usiku na Mchana vifaa vyote vipo January watapokea Wanafunzi wa kidato cha kwanza .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke Elihuruma Mabeya alisema Temeke wanajenga madarasa 207 matarajio January Temeke wanapokea Wanafunzi Elfu 23 hatua za Ujenzi nzuri Chamazi wanajenga madarasa ya kawaida na Dovya wanajenga golofa .
Mwisho