Home Uncategorized MHE. OMAR SHAABAN ATOA NENO KWA WAFANYABIASHARA AKIFUNGUA MAONESHO YA VIWANDA JIJINI...

MHE. OMAR SHAABAN ATOA NENO KWA WAFANYABIASHARA AKIFUNGUA MAONESHO YA VIWANDA JIJINI DAR

Na: Mwandishi Wetu, DSM 

Waziri wa biashara na maendeleo ya viwanda Zanzibar Mhe. Omar Shaaban amewataka wafanyabiashara kuthamini bidhaa zinazozalishwa nchini ili kuzidi kukuza uchumi wa nchi ya Tanzania.

Mhe. Omary ameyasema hayo leo Disemba 4,2022 alipokuwa akifungua rasmi maonyesho ya Saba ya bidhaa za viwanda na biashara  yanayofanyika katika viwanja vya mwalimu Julius Nyerere (sabasaba) Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa watanzania wote wanapswa kuunga mkono Jitihada za wafanyabiashara wa ndani ambapo kwa kufanya hivyo kutazidi kuimarisha  uchumi wa mfanyabiashara mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Sekta ya viwanda ni nyenzo kubwa Sana ya maendeleo katika kunyanyua uchumi wa nchi ili kuhakikisha uwekezaji katika sekta mbali mbalimbali nchini” amesema Shaban.

Aidha Waziri huyo amewataka wafanyabiashara wanaoshiriki kwenye maonesho hayo kuweka utaratibu wa kutembelea mabanda mengine ili kuweza kujifunza na kubadilishana uzoefu na kwamba kwa kufanya hivyo wataweza kubadilishana uzoefu wa kibiashara na masoko.

“Nimepata fursa ya kutembelea mabanda ya washiriki na nimejionea mwenyewe bidhaa zilizopo changamoto ni chache lakini ni vyema kuweza kuzifanyia marekebisho kwa kukaa pamoja ili kuweza kufikia lengo la kuthamini vya kwetu”

“Tuache kununua bidhaa za watu wa nje tunatakiwa tununue za kwetu Kama hakuna ndio tununue za nje lakini Cha kwetu kwanza.” amesema Shaban.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tan Trade Bi. Latifa khamis akizungumzia Maonesho hayo amesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la washiriki kwa mwaka huu kulinganisha na mwaka uliopita  2021.

“Jumla ya washiriki 502 wameweza kushiriki kwenye maonesho haya wakati mwaka Jana kulikuwa na walishiriki 121. Kila siku ya maonyesho haya kutakuwa na vikao na wafanyabiashara ili kuweza kujadili changamoto zao katika uboreshaji wa bidhaa,”amesema Latifa.

Katika hatua nyingine Bi. Latifa Khamis ameelezea mfumo mpya kwa kuandaa App kwaajili ya kuwawezesha wakulima kujua Bei ya bidhaa akiwa mahali popote atakapokuwa, na kufafanua kuwa mfumo huo utatumia simu yoyote ya mkononi bila kujali aina ya simu atakayokuwa nayo mkulima.

“Mfumo huu utamuwezesha mkulima kupata taarifa mbalimbali za bei ya mazao kwa kutumia simu yake ya mkononi iwe simu janja au kiswaswadu” amefafanua Bi. Latifa.

Maonesho hayo yaliyofunguliwa rasmi leo Disemba 4,2022 yamebebwa na kaulimbiu ya ‘Nunua bidhaa za Tanzania Jenga Tanzania’  na yanatarajia kufikia tamati Disemba 9 mwaka huu.

Previous articleWAZAZI KATA ILALA YATOA ONYO KWA WAZAZI KUTORUHUSU MGENI KULALA NA WATOTO 
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMATATU DISEMBA 5-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here