DAR ES SALAAM.
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena amesema sera ya habari ya Mwaka 2003 itaathiriwa na mabadiliko ya sheria ya habari.
Amesema, sheria yoyote ikitofautiana na sera, sera hulazimika kubadilishwa ili kukidhi haja ya sheria.
Meena ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipohojiwa na Gazeti la Mwanahalisi Jijini Dar es Salaam juu ya uwepo wa sera hizo kama zitaendana na Sheria ya habari inayotarajiwa kupelekwa Bungeni mwezi Januari 2023 ili kufanyiwa marekebisho.
Katika mahojiani hayo Meena amesema kuwa katika mchakato wowote wa kutunga sheria, Sera huwa inatangulia kwanza na baadaye sheria inafuata.
“Kimsingi Mabadiliko yanayofanywa kwenye Sheria lazima yaathiri Sera iliyopo sababu haiwezi kukiuka Katiba na Sera “ amesema Meena.
Aidha amesema kuwa endepo kama Kuna mahali marekebisho yamefanywa kwenye Sheria na yakakinzana na sera lazima sera hiyo ibadilike ili iweze kuendana na Sheria iliyopo.
“Lakini pia kama kuna mahali marekebisho yamefanywa kwenye Sheria na yakakinzana na sera lazima sera ibadilike ili iweze kuendana” amesema Meena.
Hivi karibuni Waziri mwenye dhamana ya Habari Nape Nnauye akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Sekta ya inchini Jijini Dar es Salaam alizungumzia nia ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwasilisha Bungeni muswada wa marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ili kupitiwa upya na kufanyika marekebisho katika vifungu vyenye utata katika sheria hiyo.