Na Heri Shaaban (Ilala)
MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli amepongeza kasi ya Ujenzi wa Madarasa Jimboni Segerea
Mbunge Bonah alitoa pongezi hizo katika ziara ya sekta ya Elimu jimboni Segerea kuangalia Miundombinu ya Elimu kwa ajili ya maandalizi ya kidato cha kwanza.
“Nampongeza Rais wa Jamhuri ya MUUNGANO wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika Jimbo langu la Segerea kuelekeza fedha za madarasa na Ujenzi unaenda kwa kasi “alisema Bonah
Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli, alipongeza Madiwani wa Jimbo la Segerea ambao wamefanikiwa kupata shule hizo watoto watafaulu Jimbo la Segerea watasoma katika Kata zao zilizopo jimboni .
Bonah aliwataka wazazi kuhakikisha Watoto wanasoma Elimu ya Msingi mpaka Sekondari ni Bure bila malipo
Katika hatua nyingine Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli, amempongeza Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Kinyerezi Mpya kwa usimamizi mzuri wa Shule na Miradi ya serikali .
Diwani wa Kata ya Kiwalani Mussa KAFANA alisema pochi la mama limefunguka milioni 180 walizopata mwaka jana wameweza kujenga madarasa ya kidato cha kwanza na kidato Cha pili shilingi milioni 30 wamefanya ukatabati shule ya mwale.
Kwa upande wake Msimamizi wa Ujenzi wa shule ya Sekondari ya golofa la Liwiti Idd Salehe alisema wanajenga madarasa 20 baadhi ya madarasa yatakamilika Desemba mwaka huu Ili watoto waweze kusoma January
Katika ZIARA hiyo ya kuangalia miundo mbinu ya Elimu Mbunge Bonah,alitembelea Kata ya Kinyerezi ,shule ya Kisungu ,Kinyerezi Mpya,Liwiti na Kiwalani .
Mwisho