Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Adenor Leonardo Bacchi (Tite) ameacha rasmi kazi ya kuifundisha timu hiyo baada ya kushindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 baada ya kupokea kichapo na kuondolewa kwenye michuano hiyo na Croatia.
Mwalimu huyo mkongwe raia wa Brazil alikuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa zaidi ya miaka 5 tangu alipochukua majukumu ya kuinoa timu hiyo mwaka 2016.
Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Russia, timu hiyo ya taifa ya Brazil ilicheza Michuano hiyo na kuishia hatua ya Robo Fainali baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Ubelgiji.
Licha ya kuwa na kizazi maarufu kwa sasa ulimwenguni, kina Neymar Jr, Richarlison, Rafinha, Vinicius Jr na wengine, Brazil wameshindwa kutamba katika Michuano hiyo na kutupwa nje na Croatia katika hatua hiyo ya Robo Fainali kwa changamoto ya mikwaju ya Penalti 4-2, baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 120’ za mchezo huo.