Home LOCAL KIPAUMBELE KIKUBWA KATIKA SERIKALI NINAYOIONGOZA NI KUFIKIA UCHUMI WA BULUU -DKT MWINYI

KIPAUMBELE KIKUBWA KATIKA SERIKALI NINAYOIONGOZA NI KUFIKIA UCHUMI WA BULUU -DKT MWINYI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kipaumbele kikubwa hivi sasa katika serikali anayoiongoza ni kufikia uchumi wa buluu.

Ameyasema hayo Leo Ikulu Zanzibar wakati alipokutana na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB).

Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa pia na Waziri Ofisi ya Rais  Fedha na Mipango  Dk.Saada Mkuta Salum.

Rais Dk.Mwinyi amesema kwa Sasa serikali inafanya mageuzi makubwa ya kiuchumi kupitia rasilimali zilizopo za bahari.

Amesema kwa sasa serikali inatarajia kutumia vema rasilimali hizo ili kufikia azma ya mageuzi hayo ya kiuchumi ambapo tayari sera ya uchumi wa buluu imeshatengenezwa.

Amesema malengo hayo yanategemea sana uwepo wa miundombinu ya Barabara,bandari,maji na nishati ya uhakika ya umeme hivyo maeneo hayo kwa Sasa ndio kipaumbele katika serikali.

Mbali na hayo,Rais Dk.Mwinyi ameishukuru benki ya AfDB kwa kuwa tayari kusaidia Zanzibar msaada wa kifedha katika bajeti yake pamoja na eneo la afya.

Meneja wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB),Patricia Laverley amesema benki hiyo inatambua jitihada kubwa za mageuzi ya kiuchumi zinazozifanya na Rais Dk.Mwinyi kupitia mwelekeo wa uchumi wa buluu.

Amesema kupitia mwelekeo huo wa uchumi wa buluu ambao kwa kiasi kikubwa una rasilimali za kutosha za baharini utawanufaisha wanzanzibari katika eneo la uvuvi,kilimo Cha zao la mwani na viwanda.

Amesema benki ya AfDB ipo tayari kusaidia eneo la afya ambalo Rais Dk.Mwinyi ameliwekea kipaumbele

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here