Home Uncategorized KAMISHNA MWAKILEMA ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA KUFANYA KAZI ZENYE TIJA

KAMISHNA MWAKILEMA ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA KUFANYA KAZI ZENYE TIJA

Na: Mwandishi Wetu, Arusha.

Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), William Mwakilema ameelekeza viongozi wa shirika kushirikiana na watendaji wengine katika kupanga mikakati ya pamoja ya kazi ili kuleta ufanisi.

Kamishna Mwakilema ameyasema hayo leo alipokuwa akimuapisha Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, James Paschal Kidubo anayesimamia ukaguzi wa ndani katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha.

“Washirikisheni watendaji wengi mnaofanya nao kazi ili kuwa na mikakati ya pamoja. Siku zote maamuzi yanayozingatia maoni ya watalaamu huwa yana tija” alisema

“Utafanya maamuzi kama kiongozi lakini kwa kushirikisha watendaji wengine itafanya kazi yako iwe nyepesi” alisisitiza Kamishna Mwakilema.

Kwa upande wake Kamishna James Paschal Kidubo aliahidi kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana na watendaji wengine. “Natambua majukumu haya ni makubwa na ninaahidi kupokea na kufanyia kazi maoni na ushauri kutoka kwa wasaidizi wangu na pia maelekezo kutoka kwa viongozi.” alisema.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Richard Kafwita alisema Kamishna Kidubo ana elimu ya Shahada ya Uzamili katika masuala ya fedha (Master of Science in Finance) kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde nchini Uingereza kwa ushirikiano na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es salaam, Tanzania na ana Cheti cha Uhasibu (CPA). Kamishna Kidubo aliajiriwa TANAPA tangu mwaka 2013.

Previous articleSERENGETI BYTES YATANGAZA MSIMU WA TATU WA TUZO ZA KIDIGITALI TANZANIA
Next articleRC MAKALA AZUIA WATENDAJI TEMEKE KUSAFIRI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here