Home Uncategorized CHUO CHA BAHARI (DMI) CHAOMBA MIUNDOMBINU YAKE IKARABATIWE

CHUO CHA BAHARI (DMI) CHAOMBA MIUNDOMBINU YAKE IKARABATIWE

Meja Jenerali mstaafu, Said Shaaban ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) akizungumza wakati wa kusanyiko la wahitimu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), lililofanyika leo chuoni hapo Posta Dar es Saklaam.

Baadhi ya washiriki wa kusanyiko la wahitimu wa DMI wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wataalamu wa chuo hicho kuelekea mahafali yanayofanyika siku ya Alhamisi chuoni hapo.

Mgeni rasmi Meja Jenerali mstaafu, Said Shaaban ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya kusanyiko la wahitimu wa DMI

Mgeni rasmi Meja Jenerali mstaafu, Said Shaaban ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa  Chuo cha Bahari DMI waliofanya vizuri kwenye masomo yao.

Mgeni rasmi Meja Jenerali mstaafu, Said Shaaban ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) akiwa kwenye picha ya pamoja nawafanyakazi wa DMI

·    Yasema ubora wa chuo haulingani na miundombinu yake

·    Yajivunia kutoa wahitimu bora wa fani mbalimbali

Na Mwandishi Wetu

CHUO cha Bahari Dar es Salaam, (DMI), kimeomba serikali ikipatie meli ya mafunzo kwaajili ya kuwaongezea ujuzi wahimu wa mafunzo chuoni hapo na kimeomba miundombinu ya chuo hicho ikarabatiwe ili kwenda na wakati.

Ombi hilo limetolewa na Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Dk. Tumaini Gurumo wakati akizungumza kwenye kusanyiko la wahitimu wa chuo hicho ambalo limefanyika chuoni hapo Posta Dar es Salaam.

“Uzuri wa meli ya mafunzo inakuwa imetengenezwa maalum kwaajili ya mafunzo, inakuwa na madarasa na vyumba vya kulala mle na unaweza kuifanya ya biashara ukaingiza fedha na wakati huo huo ya mafunzo hivyo uendeshaji wake ukawa rahisi kidogo kwasababu kumiliki meli siyo rahisi sana

“Kwa hiyo tukipata meli ya aina hiyo hata kama itakuwa inasafirisha kontena kutoka Tanzania kwenda nchi zingine itasaidia kupata nafasi za mafunzo kwa wanafunzi wetu na hivyo kupata mabaharia wengi sana hapa nchini,” alisema

Aidha, Dk. Tumaini alisema mahitaji ya mabaharia ni makubwa sana lakini wengi wanaohitimu mafunzo ya nadharia wako mitaani wakisubiri kupata mafunzo ya vitendo ili waweze kukamilika.

 Alitaja changamoto inayokabili chuo hicho kuwa ni uchakavu wa miundombinu kwani kimekuwa kikitumia miundombinu ile ile ya miaka ya 80 tangu kianzishwe kikiwa na wanafunzi 12 na inaendelea na miundombinu hiyo hiyo kikiwa na wanafunzi 4,049.

“Kwa hadhi ya wataalamu tunaozalisha hapa DMI na kwa maendeleo ambayo dunia imepitia hadi mwaka huu 2022 hatustahili kuendelea kuwa kwenye miundombinu chakavu kama hii,” alisema 

Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Dk. Tumaini Gurumo, alisema kusanyiko la wahitimu ni muhimu kwaajili ya kuwatambua wahitimu waliowahi kusoma kwenye chuo hicho sehemu walipo kwa sasa.

“Tunawakusanya na kuwasajili tunawaeleza chuo chao walichosoma kiko katika hali gani na tunawaeleza mipango yetu ya mbeleni na wao wanapata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu kile walichokiona wakiwa wanasoma na hali ilivyo sasa na kushauri wapi tuelekee,” alisema Dk.  Tumaini

Alisema kupitia kusanyiko hilo watajadili changamoto ya muda mrefu sana ya mafunzo ya vitendo kwa wahitimu wa chuo hicho ambayo huwa yanafanyika kwenye meli.

Dk. Tumaini aliishukuru serikali kwa kuendelea kuipa vifaa vya kufundishia na wahitimu kufanya mafunzo ya vitendo ambavyo hata hivyo bado havijakidhi mahitaji ya sasa ya wahitimu waliopo.

“Mtambo wa kufundisha wanafunzi kuendesha meli Stimulators ni muhimu kwa wahitimu kwani ndio unamwonyesha mhitimu kila kilichoko kwenye meli lakini pia mwisho wa siku lazima mhitimu aingie kwenye meli  lakini inashindikana kwasababu hapa nchini hakuna meli za kutosha,” alisema

Aidha, alisema kama kungekuwa na meli nyingi za hapa nchini ingekuwa rahisi kuweka viwango kwa kila meli kuchukua kiasi cha wahitimu watano kwaajili ya mafunzo ya vitendo lakini fursa hiyo haipo.

“Tunategemea meli za nchi zingine zichukue wahitimu wetu kwaajili ya mafunzo ya vitendo huwa siyo rahisi sana kwasababu hizo meli zinakuwa nanafasi chache sana. Na ilimhitimu aive vizuri lazima apate mafunzo ya kwenye meli,” alisema

“Tunahitaji watu wa kutusemea huko kwenye vikao kwamba Tanzania imeingia makubaliano na baadhi ya nchi sasa yakitekelezwa vijana wetu watapata fursa nyingi za kufanya mafunzo ya vitendo,” alisema.

Wakati huo huo chuo hicho kimepongezwa kwa kutoa Shahaza za Uzamili katika usafiri wa maji hali ambayo itasaidia kupata wataalamu wengi wa sekta ya usafiri wa majini.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Meja Jenerali mstaafu, Said Shaaban ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) wakati akizunyumza kwenye kusanyiko hilo.

Alisema tangu kuanzishwa kwake chuo hicho kimefanikiwa kutoa wahitimu wengi wanaofanya kazi ndani na nje ya nchi katika sekta ya usafiri wa majini.

“Mahitaji ya wataalamu wa bahari bado ni makubwa sana hapa nchini ndiyo maana naona mchango wa DMI ni mkubwa sana katika kupata watu watakaofanyakazi kwenye usafiri wa majini ndani na nje ya nchi,” alisema

Previous articleNAIBU WAZIRI WA FEDHA ATOA WITO KWA WAWEKEZAJI KUENDELEA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO TANZANIA
Next articleWABUNIFU KUTAMBIANA JUKWAA LA RUNWAY BAY ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here