Home BUSINESS BODI YA EWURA YAFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MIUNDOMBINU YA KUHIFADHIA MAFUTA...

BODI YA EWURA YAFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MIUNDOMBINU YA KUHIFADHIA MAFUTA TIPER

Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), leo Tar.20/12/2022, imefanya ziara ya kikazi katika miundombinu ya kuhifadhia mafuta ya TIPER (Tanzania International Petroleum Reserves Ltd) iliyopo eneo la Kigamboni, Dar es Salaam, ili kujionea kazi, maendeleo na changamoto mbalimbali zinazoikabili Kampuni hiyo katika uhifadhi wa mafuta.

Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof. Mark Mwandosya, ameeleza kwamba, EWURA kama mdhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, imefanya ziara hiyo ili kufahamu kiundani utekelezaji wa majukumu ya uhifadhi wa mafuta nchini, kujua mafanikio na changamoto mbalimbali, ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na tija kwa taifa kwa ujumla.

Aidha, akifanya wasilisho juu ya Utendaji wa Kampuni hiyo, Kaimu Meneja wa TIPER, Bw. Martin Mosha alisema:

”TIPER ipo kimkakati kuhakikisha nchi inakua na hifadhi ya mafuta ya kutosha kwa matumizi ya nchini na baadhi ya nchi zinazotegemea kupitisha mafuta nchini kama vile Zambia, Kongo, Malawi, Burundi”

Kwasasa TIPER ina eneo lenye ukubwa wa hekta 58 na maghala 32 yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 253 za mafuta, ikiwa zimeongezeka kutoka lita milioni 140 wakati Kampuni hiyo inaanza kazi mwaka 1999.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here