Home LOCAL BARABARA YA MAKETE – MBEYA KUFUNGUKA KWA LAMI

BARABARA YA MAKETE – MBEYA KUFUNGUKA KWA LAMI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa wananchi wa Wilaya ya Makete, Mkoani Njombe, kabla ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami Wilayani Makete.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw, Antony Mtaka, kabla ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa barabara yaKitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami Wilayani hapo, Mkoani Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw,Antony Mtaka, akiwasilisha taarifa ya Mkoa huo kabla ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami, iliyofanyika Wilayani Makete Mkoani Njombe.
Mbunge wa Makete Mhe. Festo Sanga akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Makete kabla ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami, iliyofanyika Wilayani Makete, Mkoani Njombe.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila akiwa na Muwakilishi wa Kampuni ya M/S China National Aero-Technology Engineering Corporation (wa pili kulia) wakionyesha mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami, mara baada ya kuusaini Wilayani Makete, Mkoani Njombe.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wakala wa Barabaraa Nchini (TANROADS) mara baada ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 kwa kiwango cha Lami Wilayani Makete, Mkoani Njombe (PICHA NA WUU).
NJOMBE

Barabara ya Makete-Mbeya kufunguka kwa lami Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara za lami katika mikoa ya nyanda za juu kusini ili kuunganisha vema ukanda huo na bandari ya Mtwara na hivyo kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji, kukuza uzalishaji wa mazao ya kilimo, misitu na kukuza utalii.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini ujenzi wa barabara ya Isyonje-Kikondo hadi Makete KM 96.2 sehemu ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami Waziri Prof. Mbarawa amesema Serikali ya awamu ya sita itahakikisha inaunganisha kwa njia fupi mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Njombe hadi Mbeya kupitia Makete ili kukuza fursa za kiuchumi zilizoko katika ushoroba huo.
“Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia imejikita kwenye kuboreshamiundombinu hususani maeneo yenye uzalishaji mkubwa hivyo niwahakikishie kuwa ongezeni uzalishaji miundombinu bora inakuja,’ amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Ameitaka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kumsimamia kikamilifu Mkandarasi anayejenga barabara hiyo M/S China National Aero-Technology Egineering Corporation ili mradi huo ukamilike kwa wakati na viwango.

Mtendaji mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila amesema ujenzi wa barabara hiyo utahusisha ujenzi wa mizani katika Kijiji cha Igalala ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito hivyo kuwataka wananchi kuzingatia sheria na kulinda miundombinu yote ya barabara.Kwa upande wake Mbunge wa Makete Festo Sanga ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo kwani kukamilika kwake kutaunganisha wilaya hiyo na Mkoa wa Mbeya kwa njia fupi, kukuza utalii wa hifadhi ya taifa Kitulo na kupandisha thamani ya mazao mbalimbali yanayozalishwa Mkoani Njombe.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Bw, Anthon Mtaka amewataka wakazi wa wilaya ya Makete kote nchini kutumia maendeleo ya ujenzi wa miundombinu kuwekeza wilayani humo. Zaidi ya shilingi bilioni 69.7 zinatarajiwa kutumika katika
ujenzi huo unaotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 6.
Previous articleMAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KUMJULIA HALI LOWASSA
Next articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI DISEMBA 29 -2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here