Home LOCAL AMEWATAKA WALIMU KUTOKOMEZA ZIRO ILALA 

AMEWATAKA WALIMU KUTOKOMEZA ZIRO ILALA 

Diwani wa Viti Maalum Wanawake Ilala Mwalimu Beatrice Edward

Diwani wa Viti maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Aisha Kipini akizungumza na katika kikao Cha Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Ilala .Na Heri Shaaban.

Na: Heri Shaaban(Ilala )

Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Mwalimu Beatrice Edward amewataka walimu Ilala kufanya kazi kwa weledi kushirikiana na Walimu kutokomeza ZIRO.

Mwalimu Beatrice ametoa ushauri huo katika kikao cha Kamati ya Maendeleo Kata ya Ilala kilichokuwa kinajadili Maendeleo .

“Nawaomba Walimu wenzangu tushirikiane na wazazi katika Sekta ya elimu kuisaidia Serikali kutokomeza ZIRO Ilala iweze kuwa juu kwenye Eimu” alisema Mwalimu Beartice

Aliwataka Walimu kuendelea kusimamia maadili kwa Wanafunzi wawapo shuleni na Walimu wa shule za Sekondari kuiga mfano Elimu Msingi katika jitihada za kuongeza ufaulu

Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Aisha Kipini, aliwataka Wazazi kutenga muda kuzungumza na watoto wao wawe marafiki kila wakati kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili .

Aidha Diwani Aisha alipiga MARUFUKU wazazi kutuma watoto sokoni na dukani nyakati za usiku kwani ulimwengu umebadilika watu wanawafanya vitendo Vya ukatili watoto .

Mwisho.

Previous articleWANAFUNZI WA VIJIJI VYA KITANGE, KITANGE ONE NA KIJIJI CHA USUNGU WILAYANI KILOSA WANATEMBEA UMBALI WA KILOMETA 36 KUFUATA SHULE.
Next articleWAZAZI WAASWA KUWEKA MSUKUMO WA KUTOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA VIJANA   SHULENI KUEPUSHA MIMBA ZA UTOTONI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here