Home LOCAL WAZIRI MKUU AIPONGEZA WIZARA YA AFYA KUTEKELEZA MAAGIZO YA KUKAMILIKA UJENZI WA...

WAZIRI MKUU AIPONGEZA WIZARA YA AFYA KUTEKELEZA MAAGIZO YA KUKAMILIKA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KATAVI.

Katavi , 12 Disemba 2022

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameipongeza hatua ya Wizara ya Afya ya kuongeza kasi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi baada ya kutekelezwa maagizo yake ya kushirikiana na Ofisi ya Mkoa katika kusimamia mradi huo ambayo maagizo hayo aliyatoa mwaka jana 2021 mwezi wa nane .

Katika ziara yake Mkoani Katavi, Waziri Mkuu ametembelea Hospitali hiyo na kukuta ujenzi sasa umefikia asilimia 92 kwa ‘Wing A’ kutoka asilimia 40 mwaka jana.

Akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema kuwa mradi wa Wing A utakamilika 31 Desemba, 2022 na huduma kuanza kutolewa tarehe 01 Januari, 2023 .

Prof. Makubi amesema Ujenzi wa Wing B unategemea kukamilika Oktoba, 2023. Mheshimiwa Waziri Mkuu yupo Mkoani Katavi kwa ziara ya siku mbili.

Previous articleRC MAKALA AMEWATAKA WATENDAJI WAKIAMKA WAWAZE UJENZI WA MADARASA
Next articleYETU MICROFINANCE BANK PLC KUWEKWA CHINI YA USIMAMIZI WA BENKI KUU YA TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here