Home SPORTS YANGA YAENDELEZA UBABE WA SHINDI, YAIPIGA KAGERA SUGAR 1-0 KIRUMBA

YANGA YAENDELEZA UBABE WA SHINDI, YAIPIGA KAGERA SUGAR 1-0 KIRUMBA

Timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa goli 1-0 kwa kuitandika timu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Katika mchezo uliopigwa Leo Novemba 13,2022 katika Dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza

Goli pekee la Yanga limepachikwa wavuni na Clement Mzize  alipounganisha  krosi safi kutoka kwa Feisal Salum  na kupachika wavuni kwa kichwa.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Yanga ilikuwa ikiongoza kwa goli hilo.

Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi kwa timu zote mbili huku Mtibwa Sugar wakionekana kulishambulia lango la Yanga katika vipindi vyote viwili lakini hadi filimbi ya mwisho inapulizwa wameshindwa kuziona nyavu za miamba hiyo ya Jangwani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here