Home BUSINESS WIZARA YA UWEKEZAJI YASAINI MKATABA WA KUBORESHA SERA YA VIWANDA NA BIASHARA...

WIZARA YA UWEKEZAJI YASAINI MKATABA WA KUBORESHA SERA YA VIWANDA NA BIASHARA NDOGO NCHINI

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara yasaini hati ya makubaliano (MOU) na taasisi ya Tanzania Startup Apex (TSA) kwa lengo la kuboresha sera ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo kwa ajili ya biashara mpya.

Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini hati ya makubaliano iliyofanyika leo tarehe 9 Novemba, 2022 katika ofisi za Wizara Mtumba.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Aristides Mbwasi amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuboresha mazingira ya biashara hasa kwa kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha Sera zote zinazohusu biashara Ndogo na za Kati zinaboreshwa ili kusaidia maendeleo ya biashara nchini.

Bw. Mbwasi ameongeza kuwa lengo la Wizara kuingia makubaliano na TSA ambayo ni sekta binafsi ni kujenga mazingira bora ya uanzishwaji na uendelezaji biashara kwa wajasiriamali wadogo na wa Kati hasa biashara mpya.Awali akieleza mchakato wa makubaliano hayo na hatua iliyopitia.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Viwanda Vidogo na Vya Kati Bw. Wilfred Kahwa amesema kuwa Wizara inashirikiana na TSA katika mambo yenye maslahi yanayofanana yanayolenga uboreshwaji wa sera za kisekta na mikakati na programu mbalimbali zinazolenga uongezaji wa fursa za uwekezaji na maendeleo ya wajasiriamali.

Naye Mwakilishi wa taasisi ya Tanzania Startup Apex (TSA) Bw. Michael Mushi ameishukuru Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa ushirikiano ilioonesha katika kufikia hatima ya makubaliano hayo.

Aidha Bw. Mushi amesema kuwa kazi kubwa ya TSA ni kuzisaidia kampuni changa kwa kutengeneza sera nzuri kwa ajili ya biashara Ndogo na za Kati kwani ndizo zinazochangia kwa kiasi kikubwa ajira na uchumi wa Nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here