Home LOCAL WAZIRI NAPE: SERIKALI IMEPOKEA MAONI YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA HUDUMA ZA...

WAZIRI NAPE: SERIKALI IMEPOKEA MAONI YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI

Na: Mwandishi Wetu.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia Mhe. Nape Nnauye amewahakikishia Wadau wa Sekta ya Habari kuwa Serikali imepokea maoni yao kuhusu marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari Na 12 ya 2016.

Ameyasema hayo leo Novemba 21, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na wadau hao kilicholenga kupokea maoni yao.

“Niwahakikishie kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan inayo nia ya dhati katika jambo hili.” alisisitiza Waziri Nape

Akieleza zaidi Waziri Nape amesema kuwepo kwa vikao na wadau ni ishara kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inania na dhamira njema kwa sekta ya habari.

“Nimekuja mwenyewe kuwasilikiliza na imani yangu ni kuona sekta inaendelea kukua” ameongeza Waziri Nape.

Wadau walioshiriki kikao nicho ni pamoja na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Chama wa Waandishi wa Habari Tanzania (JOWUTA) na MISA- Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here