Home LOCAL WATENDAJI WA KATA, VIJIJI KITANZINI LISHE YA WANAFUNZI MASHULENI

WATENDAJI WA KATA, VIJIJI KITANZINI LISHE YA WANAFUNZI MASHULENI

Kikao cha Kamati ya Lishe wilayani Serengeti kimewataka watendaji wa kata na vijiji kusimamia kikamilifu afua za lishe mashuleni kwa kushirikiana na kamati za shule na kuhamasisha wazazi na walezi kupitia vikao na mikutano mbalimbali.

Hayo yameazimiwa katika kikao cha robo ya kwanza cha lishe kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti,akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa kamati ya Lishe ambae ni pia Mkurungenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Ndg Kivuma H. Msangi amesema katika tathimini iliyofanyika ya programu ya utoaji wa huduma za chakula na lishe mashuleni wilaya ya Serengeti ina asilimia 29.61,ambapo kati ya shule 179 ni 53 zinatoa chakula kwa wanafunzi shuleni hivyo ikionesha eneo ilo wilaya haifanyi vizuri.

Ameongeza pia katika kuhakikisha wanafunzi wanapata utulivu wa akili na afya ni muhimu watendaji wa kata na vijiji kwa kushirikiana na viongozi wote wakiwemo wa shule wanalivalia njuga swala la lishe mashuleni ili utendaji wa wilaya uwe kwa asilimia 100 kwenye eneo hilo.

Nae Mganga Mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt.Emiliana Donald amewashukuru viongozi na shule ambao wamelipa kipaumbele swala hilo la lishe na kuwaomba kuibeba ajenda hiyo ya lishe kwenye mikutano ya hadhari na maeneo mbalimbali.

Kamati imewasisitiza wazazi kuwa mstari wa mbele katika swala la lishe na chakula kwa ajili ya watoto wao wawapo shuleni na kuitaka kila shule kuandaa mpango kazi wa lishe na chakula na kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kikamilifu.

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti imeendelea kujizatiti na kuongeza juhudi katika kuimarisha afua mbalimbali za Lishe ambapo katika tathimi ya Robo ya Kwanza ‘’score card’’ katika upande wa ziara za usimamizi vituoni kuhusu masuala ya lishe 100%,watoto waliopata walipatiwa nyongeza ya matone ya vitamini A Jumla ya watoto 70948 kati ya watoto 70677 sawa na 100%, Jumla ya akina mama/Walezi 36,325 kati ya 36,760 walipatiwa elimu ya Afya kutoka kwa watoa huduma za Afya sawa na 98.8%, Jumla ya mitaa na vijiji 72 viliazimisha siku ya afya na lishe kati ya 101 sawa na 71.3%, Jumla ya akina mama/Walezi 20,071 kati ya 8,645 walipatiwa elimu ya Afya ngazi ya jamii sawa na zaidi ya asilimia 100, Utoaji wa dawa za kuongeza damu (IFA) kwa akina mama wajawazito umefanyika kwa 91.4%. Kina mama 14,589 wamepatiwa dawa za kuongeza damu kati ya 15,967.Aidha Wilaya itaendelea kuongeza juhudi wenye utekelezaji wa shughuli za lishe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here