Home BUSINESS WANANCHI WASHAURIWA KUJIEPUSHA NA MIKOPO UMIZA

WANANCHI WASHAURIWA KUJIEPUSHA NA MIKOPO UMIZA

Meneja Msaidizi wa Uhusiano Kwa Umma Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Noves Mosses (kushoto) akiwakabidhi zawadi wanafunzi wa Chuo Kikuu cha SaUT walipotembelea katika Banda la Benki hiyo kupata elimu maonesho ya wiki ya huduma yaliyomalizika rasmi Novemba 26,2022 Jijini Mwanza.

Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya fedha (BoT) Ephraim Madembwe (kushoto) akitoa elimu kwa Kundi la wana chuo walipotembelea kwenye Banda la taasisi hiyo kupata elimu. Maadhimisho hayo yamefungwa rasmi Novemba 26, 2022 Jijini Mwanza.

Meneja Msaidizi upatikanaji na usimamizi wa akiba ya fedha za kigeni Dkt. Anna Lyimo (kushoto) akitoa elimu kwa kijana aliyetembelea Katika Banda la Benki hiyo kupata elimu ya fedha na kufahamu shughuli za Benki hiyo

Maafisa wa BoT wakisikiliza kwa .akini maswali yaliyokuwa yakiulizwa na mwananchi aliyetembelea katika Banda lao kwaajili ya kupata ufafanuzi. (wa kwanza kushoto) ni Afisa Sheria wa Benki hiyo happy Mlwale (wapili kushoto) ni Meneja Msaidizi elimu ya fedha na Mwenendo wa masoko, Khadija Kishimba, (wa tatu aliyesimama) ni Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha Deogratias Mnyamani , na (wa mwisho) ni, Afisa Mwandamizi wa taasisi hiyo Gideon Rwegoshora.

Afisa Mwandamizi wa BoT Gideon Rwegoshora (wa pili kushoto) akizungumza kutoa elimu ya fedha kwa mgeni aliyetembelea katika Banda la taasisi hiyo kupata elimu. ( Kwanza kushoto) ni, Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha Deogratias Mnyamani

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Imewataka watanzania kufanya tathinini ya riba za mikopo inayotolewa na taasisi za fedha hapa nchini kabla ya kwenda kuomba mikopo kwenye taasisi hizo ili Kuondokana na changamoto ya kushindwa  kurejesha mikopo hiyo 

Hayo yamebainishwa na Meneja Msaidizi wa Uhusiano Kwa Umma BoT Noves Mosses katika maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha yaliyomalizika rasmi Novemba 26,2022 katika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza.

Amesema wananchi wengi wamejikuta wakiangukia kwenye mikopo yenye riba kubwa kutokana na ukosefu wa elimu ya kutosha katika maswala mbalimbali ya kifedha na matokeo yake kushindwa kumudu kurejesha mikopo hiyo.

Amesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania  imetumia fursa ya uwepo wa maonesho hayo kutoa elimu kwa wanchi ambapo nao  wameweza kukutana na taasisi mbalimbali za kifedha zilizoshiriki katika maonesho hayo.

Aidha, ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo wamebaini uwepo wa wananchi wengi kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya masuala ya kifedha na kwamba Benki hiyo itaendelea kutoa elimu ya mara kwa mara Ili wananchi wengi zaidi waweze kufikiwa na elimu hiyo.

“Tunawashauri wananchi wote kwenda kwenye Taasisi za Kifedha zilizosajiliwa na BoT ili kujiepusha na Mikopo yenye riba kubwa na kufanya tathimini ya riba inayotozwa katika mikopo hiyo ili kujiridhisha kabla ya kufanya maamuzi ya kukopa” amesema Noves.

Kuhusu Wiki ya Huduma za Kifedha amesema kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa wananchi katika kupata elimu ya fedha na kwamba zaidi ya wananchi 800 wamejitokeza katika Banda la BoT kupata elimu na kuomba miongozo mbalimbali ya namna ya kujihusiaha na utoaji huduma katika Sekta ya fedha.

Noves amewasihi wanachi kutembelea BoT kupata elimu na ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili katika sekta ya fedha.

Wiki ya Huduma za Kifedha ilianza rasmi Novemba 21 hadi 26, 2022 na kuhudhuriwa na Taasisi za fedha yaidi ya 100.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here