Home BUSINESS TIRA YAWAALIKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO MAONESHO YA WIKI YA HUDUMA ZA...

TIRA YAWAALIKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO MAONESHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA JIJINI MWANZA

Mwanza

Wito umetolewa kwa Wananchi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake kutembelea bandaMamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ili kupata elimu na kufahamu huduma mbalimbali za bima zinazotolewa na Taasisi hiyo katika maonesho ya wiki ya Huduma za Fedha yanayofanyika katika viwanja vya Rockcity mall, Jijini Mwanza.

Wito huo umetolewa leo Novemba 22, 2022 jijini humo na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa bima Kanda ya ziwa (TIRA) Richard Toyota, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho hayo.

Amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kufahamu umuhimu wa Bima ambayo ina lengo la kulinda maisha yao katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na maisha kwa ujumla.

Amesema kuwa maonesho hayo yanalenga kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo tofauti ya kifedha na kwamba wao kama TIRA wameshiriki ili kuweza kukutana na wananchi hao na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na Bima.

Naye Stella Rutaguza ambae Meneja wa maendeleo ya soko la Bima (TIRA), ameelezea uwepo wa fursa zilizopo kwenye maonesho hayo ambazo wao kama TIRA wanazitoa kwa wananchi kuwa ni pamoja na  kuwafundisha haki na wajibu wao juu ya taratibu za kufuata pale wanapokuwa na madai ya Bima.

Aidha Bi. Rutaguza amesema kuwa TIRA wamekuwa na utaratibu mzuri wa utoaji wa elimu kwa wananchikuhusu huduma za Bima  na kwamba hatua hiyo imesaidia kuwepo kwa ongezeko la wananchi wenye uelewa mpana juu ya umuhimu wa Bima na kwamba kuna muamko mkubwa kwa wananchi kujitokeza kujiandikisha katika Bima mbalimbali hapa nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here