Home SPORTS SINGIDA BIG STARS, SIMBA SC ZATOKA SARE

SINGIDA BIG STARS, SIMBA SC ZATOKA SARE

Wekundu wa Msimbazi Simba SC imetoshana nguvu na timu ya Singida Big stars kwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Katika mchezo huo uliopigwa leo katika Dimba la Liti, wenyeji Singida ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Simba katika dakika ya 11 ya mchezo huo likifungwa na Deus Kaseke, goli lililodumu katika kipindi chote cha kwanza.

Kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko na kuingia Piter Banda aliyebadilishana na kiungo Jonas Mkude hivyo kuifanya timu hiyo uongeza kasi na kifanikiwa kupata goli la kusawazisha katika Dakika ya 59 ya mchezo huo liipachikwa na Piter Banda.

Kufuatia Suluhu iliyopatikana katika mchezo huo timu ya Simba imeendelea kubaki katika nafasi ya pili ikiwa na alama 18 ikiwa na magoli mengi ya kufunga huku Singida ikisalia katika nafasi ya tatu kiwa na alama 18 ikiwa na magoli machache ya kufunga.

Previous article RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA MISRI KATIKA MJI WA SHARM EL SHEIKH NCHINI MISRI
Next article
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here