Kazi ya kusafisha na kupima ubora wa maji katika kisima cha kwa Gwajima kinachomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mhe. Josephat Gwajima kilichopo Majengo Salasala, kata ya Goba imekamilika kwa ajili ya kuingizwa kwenye mfumo rasmi wa usambazaji maji wa DAWASA ili kuboresha hali ya upatikanaji maji katika maeneo hayo.
Kisima hicho chenye urefu wa mita 47 kina uwezo wa kuzalisha *lita 192, 000* kwa siku. Kazi ya uboreshaji wa kisima na kuingiza maji kwenye mfumo wa usambazaji itakamilika 18/11/2022. Kisima hiki kitatumika kuboresha hali ya upatikanaji maji kwa wakazi takribani 1400.
DAWASA sasa inazalisha jumla ya lita *milioni 30.3* kwa siku kupitia visima virefu.
DAWASA inamshukuru Mhe. Gwajima kwa kujitoa na kwa kuchangia katika kuongeza wigo wa upatikanaji maji katika kipindi cha ukame.