.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Shafii Mpenda (kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga (kushoto) kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa Kituo cha Afya Mwazye kitakachoanza huduma Desemba 2022. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Tano Mwera .Jengo la zahanati ya kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo likiendelea na ukabarati baada ya kuezuliwa na upepo mwaka 2020 hivyo kupelekea Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga kuelekeza halmashauri ya Kalambo kupeleka pesa za ukarabati Kalambo kupeleka pesa za ukarabati.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akishiriki kazi ya ukarabati wa zahanati ya kijiji cha Kapozwa kata ya Mpombwe wilaya ya Kalambo jana alipokwenda kuikagua . Zahanati hiyo iliezuliwa paa lake na upepo mwaka 2020 ambapo Oktoba 20 mwaka huu wananchi walimwomba Mkuu wa Mkoa asaidie iezekwe upya.
Na. OMM Rukwa
Wananchi wa Wilaya ya Kalambo wametakiwa kuendelea kuunga mkono
jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha miradi ya maendeleo ikiwemo zahanati na vituo vya afya vinakamilika kwa wakati na kuanza kutoa
huduma.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga ametoa wito huo ( Novemba 04,2022) wakati alipofanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Oktoba 20 mwaka huu kwa uongozi wa Wilaya ya Kalambo kuhakisha miradi ya afya ya zamani inatengewa fedha na kukamilishwa .
“Nimepita kuja kujionea hali ya utekelezaji wa maalekezo yangu ambapo
nimeona tayari halmashauri imeanza kutoa fedha na kazi za kukamilisha zahanati ya kijiji cha Kapozwa, kituo cha Afya Kanyezi na Legeza mwendo zimeanza” alisema Sendiga.
Sendiga aliongeza kusema ziara zake kwenye halmashauri zinaendelea ili
kuhakikisha Rukwa inaondokana na uwepo wa miradi viporo hususan kwenye
sekta ya afya.
“Nawataka watendaji wote wa serikali kwenye mkoa huu wawajibike ili kuleta
matokeo chanya kwa kutatua changamoto za miradi ya maendeleo. Nitahakikisha ninafika maeneo yote kuwatatulia kero wananchi na kuwa hakuna changamoto katika utendaji tutashindwa kuitatua” alisisitiza Sendiga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Shafii
Mpenda akizungumza na waandishi wa habari katika kijiji cha Kapozwa alisema ataendelea kusimamia shughuli za maendeleo ikiwemo miradi iliyotolewa maelekezo na Mkuu wa Mkoa Sendiga.
Shafii aliongeza kusema nguvu za wananchi zilizotumika kutekeleza miradi ya afya itaenziwa kwa halmashauri kutoa fedha kukamilisha miradi hiyo ambapo
ametoa wito kwa awananchi kutochoka kuchangia nguvu zao .
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa Sendiga amekagua ujenzi wa kituo cha Afya Mwazye ambacho ameagiza kianze kutoa huduma mwisho wa mwezi huu
Novemba huku kituo cha Afya Kanyezi kimepatiwa shilingi Milioni Arobaini na
Kituo cha afya Legeza Mwendo kimepatiwa shilingi Milioni Sitini ili vikalimishwe kabla ya Desemba mwaka huu.