Home Uncategorized PROF. MAKUBI AKUTANA NA MKURUGENZI WA PROGRAMU ZA AFYA WA IRELAND

PROF. MAKUBI AKUTANA NA MKURUGENZI WA PROGRAMU ZA AFYA WA IRELAND

Kutoka Dodoma 9/11/202

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi leo amekutana na Mkurugenzi wa Program za Afya Wizara ya afya kutoka Ireland Prof. David Weakliam aliyeambatana na wajumbe wa Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.

Katika kikao hicho wamekubaliana kushirikiana katika maeneo ya kuboresha huduma za afya nchini, kuboresha mifumo ya afya, kushirikiana katika kutoa elimu juu ya magonjwa yasiyoyaambukiza, eneo la huduma ya afya ya mama na mtoto, rasilimali watu kwa kujengewa uwezo madaktari bingwa na bobezi Pamoja na eneo la utafiti.

#MtuNiAfya
#JaliAfyaYako

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here