Na: Heri Shaaban (Ilala)
MKUU wa wilaya ya Ilala Arch,Ng’Wilabuzu Ludigija ametoa maagizo kwa Watendaji wa Halmashauri ya Jiji kusimamia Usafi katika maeneo yao Mtendaji atakayezembea kusimamia Majukumu ya Usafi aandike Barua mwenyewe aachie ngazi.
Mkuu wa Wilaya Ilala Arch,Ng’Wilabuzu Ludigija aliyasema hayo Wilayani Ilala Leo katika kampeni endelevu ya Usafi ,Safisha Jiji la Dar es Salaam ambapo leo safisha safisha Posta mpya .
Ludigija alisema Mtendaji yoyote aliyopo Wilayani Ilala anatakiwa sasa kuunga Mkono Kampeni ya Serikali katika kusafisha na kuipendezesha jiji la Dar es Salaam liweze kuwa Bora zaidi tushike nafasi ya kwanza katika majiji ya Usafi.
“Jijl,i letu la Dar es Salaam kwa sasa tumeshika nafasi ya pili katika Usafi mikakati yetu tushike nafasi ya kwanza katika majiji Bora ya safi hivyo Watendaji wa Wilaya ya Ilala tusimamie Usafi mtendaji atakayeshindwa aandike Barua mwenyewe “ alisema Ludigija
” maelekezo yote yanayotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Wilaya ILALA wanatekeleza ikiwemo kupanga wamachinga katika utaratibu Maalum na Sasa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam linavutia kwa usafi maeneo yote wafanyabiashara wapo katika maeneo rasmi yaliopangwa.
Katika kampeni hiyo endelevu ya usafi Wilayani Ilala Kampuni mbali mbali za Usafi zinaunga mkono kampeni hiyo ikiwemo KAJENJERE TRADING CO.LTD .
Wengine waliounga mkono kampeni hiyo ya usafi Mabalozi wa Usafi Diksoni Makwaya (BAMBO) na Hamis Changaye (MTANGA)
Kwa upande wake KIONGOZI wa Wamachinga Dar es Salaam Yusuph Namoto amempongeza Usafi Jiji la Dar es Salaam kwa Sasa linavutia kasi iendelee ya kuboresha Jiji hilo.
Namoto amesema wamachinga walikosa maeneo ya Biashara wawasiliane na Ofisi yake ya Wamachinga au Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ilala nafasi zipo Bado katika masoko kauli mbiu Yetu ondoka Barabarani tukutane sokoniÂ
Mwisho