Home BUSINESS CEO BRELA APATA TUZO

CEO BRELA APATA TUZO

Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa amepata tuzo ya utendaji bora na kuwa miongoni mwa Watendaji Wakuu Bora 100 waliotunukiwa tuzo hizo kwa mwaka 2022.
 
Tuzo hiyo imetolewa tarehe 27 Novemba, 2022 katika  Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, ambapo Mkurugenzi wa Leseni kutoka BRELA Bw. Andrew Mkapa aliipokea kwa niaba yake. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar Mhe. Omar S. Shaaban (Mb).
 
Bw. Nyaisa ni miongoni mwa Wakurugenzi Wakuu na Maafisa Watendaji Wakuu sita bora wa Taasisi za Serikali ambao wamepata tuzo,  akiwemo pia Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF)  Bw. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania, Bw. Ladislaus Matindi na  Afisa Mtendaji Mkuu wa  kutoka Watumishi Housing Investment, Dkt. Fred Msemwa.
 
Akizungumza na watumishi wa BRELA katika Ofisi za  BRELA leo tarehe 28 Novemba, 2022 baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Bw. Nyaisa amesema ushirikiano anaoupata kutoka kwa watumishi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ndiyo uliowezesha kutambuliwa  na kuwa miongoni mwa Maafisa Watendaji Wakuu waliopata tuzo.
 
Bw. Nyaisa amesema tuzo hiyo iwe chachu ya utendaji bora wa kazi kwa watumishi wote  kwani   utendaji mzuri wa kazi unaofanywa na watumishi  ndiyo uliyoiwezesha BRELA kutambulika na kuchaguliwa miongoni mwa Taasisi za Serikali.
 
Hafla hiyo inayojulikana kama Tanzania Top 100 Executive Awards ambapo kwa mwaka 2022 ni mara ya pili kufanyika,  imeandaliwa na Kampuni ya Easternstar kwa kushirikiana na KPMG Tanzania na imehudhuriwa na washiriki zaidi ya 300 kutoka Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi za Tanzania Bara na Visiwani.

Previous articleNew Hit : Aggy Baby x Jamaldin ft Baddest 47 – I LIKE THAT
Next articleRAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA 10 WA JUMUIYA YA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA (UWT) LEO JIJINI DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here