Home BUSINESS BRELA YAKUTANA NA WADAU WA VYOMBO VYA UCHUNGUZI

BRELA YAKUTANA NA WADAU WA VYOMBO VYA UCHUNGUZI

Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Andrew Mkapa akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kuhusu Utekelezaji wa Kanuni za Wamiliki Manufaa kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa

Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni na Majina ya Biashara kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Meinrad Rweyemamu akiwasilisha mada kuhusu Utekelezaji wa Kanuni za Wamiliki Manufaa kwa washiriki wa mafunzo kutoka Vyombo vya Uchunguzi leo tarehe 25 Novemba, 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo ili watimize majukumu yao kwa kufuata taratibu zilizoainishwa kwa mujibu wa Sheria.

Afisa Usajili kutoa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Gift Raphael akiwasilisha mada kuhusu mchakato wa uchakataji wa maombi ya Wamiliki Manufaa mapema leo tarehe 25 Novemba, 2022 kwa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Vyombo vya Uchunguzi katika ukumbi wa Global learning Centre, uliopo Chuo cha Utumishi wa Umma, jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Andrew Mkapa (aliyeketi katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku moja kuhusu Wamiliki Manufaa kutoka Vyombo vya Uchunguzi, mara baada ya kufungua mafunzo hayo yaliyoandaliwa na BRELA tarehe 25 Novemba, 2022 katika ukumbi wa Global learning Centre, uliopo Chuo cha Utumishi wa Umma, jijini Dar es Salaam.

Wadau wa Vyombo vya Uchunguzi kutoka Taasisi za Serikali wameshiriki mafunzo ya siku moja kuhusu Utekelezaji wa Kanuni za Wamiliki Manufaa.

Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Andrew Mkapa akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa, leo tarehe 25 Novemba, 2022 jijini Dar es Salaam, amesema lengo la mafunzo hayo ni kujengeana uwezo kwa kiutendaji kama wadau na kushirikiana kwenye shughuli mbalimbali za kiutendaji kazi ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho mbalimbali ya kisheria na kimfumo kwa niaba ya Serikali na kuhakikisha kunakuwa na utoaji wa huduma bora kwa umma.

“Lengo ni kukusanya maoni na ushauri kwa ajili ya maboresho zaidi ya utekelezaji wa Kanuni za Wamiliki Manufaa ili kuboresha utendaji kazi wetu wa kila siku pamoja na kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya Uchunguzi vinapata taarifa zenye uhakika na kwa wakati,” amefafanua Bw. Mkapa.

Bw. Mkapa amesema kampuni zina umuhimu mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi, hata hivyo uzoefu unaonesha kwamba baadhi ya kampuni hutumika vibaya kwa kufanya vitendo vya kihalifu visivyokubalika kwenye jamii ikiwa ni pamoja na utakatishaji wa fedha haramu, kufadhili vitendo vya ugaidi, vitendo vya rushwa na hata ukwepaji wa kodi.

Bw. Mkapa amesema, Benki ya Dunia na Taasisi nyingine za Kimataifa zinazojihusisha na masuala ya kusaidia biashara zimejitolea kuleta mabadiliko ya hali hiyo kwa kuanzisha dhana ya Mmiliki Manufaa (Beneficial Ownership Concept) ambayo imeungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo Tanzania.

Previous articleRPC ILALA:  SEGEREA ASIYELIPA TOZO YA ULINZI FAINI LAKI TATU
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 26-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here