Home BUSINESS BRELA, ARIPO WAWATEMBELEA MAWAKALA

BRELA, ARIPO WAWATEMBELEA MAWAKALA

Pichani ni Maafisa Waandamizi kutoka Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Novemba 10, 2022 wakiwa na Mawakala kutoka Kampuni sita (6) za jijini Dar es Salaam, zinazotoa usaidizi wa Usajili wa Alama ya Biashara na Huduma pamoja na utoaji wa Hataza kwa wafanyabiashara na wavumbuzi nchini.

DAR ES SALAAM 

Maafisa Waandamizi kutoka Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), kwa kushirikiana na Maafisa Waandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Novemba 10, 2022 wamefanya ziara ya kutembelea Mawakala sita (6) wa Tanzania waliopo jijini Dar es Salaam, kuona namna ambavyo wanasajili alama za biashara, huduma pamoja na kutoa hataza kwa wafanyabiashara na wavumbuzi wa Tanzania kupitia mfumo unaosimamiwa na ARIPO na kusikiliza changamoto wanazopitia Mawakala hao pindi wanaposajili kupitia mfumo.

BRELA inaendelea kuhamasisha wafanyabiashara kusajili Alama za Biashara na Huduma pamoja na kupata Hataza ili kupewe ulinzi wa Kisheria. Mawakala waliotembelewa ni Bowmans Tanzania, AKP Laws Advocates, FB Attorneys, NexLaw, Lexglobe IP Services na Crystal Associates.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here