Home LOCAL ASILIMIA 71 YA VIFO VINATOKANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA IKIWEMO AJALI

ASILIMIA 71 YA VIFO VINATOKANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA IKIWEMO AJALI

Na. WAF – Mwanza

Watanzania wametakiwa kubadili mtindo wa maisha ili waweze kuboresha Afya kwa kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiongezeka kutokana na ajali.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Katibu Mkuu – Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya wakati akifungua rasmi maadhimisho ya wiki ya Magonjwa Yasiyoambukiza kwa kuendelea kutoa elimu pamoja na huduma ya upimaji bila malipo kwa wananchi wa mkoa huo.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani za Mwaka 2016 ambazo zinaonesha kuwa Magonjwa yasiyoambukiza yanachangia zaidi ya vifo milioni 41, ambayo ni sawa na asilimia 71 ya vifo vyote.

“Jambo linalotia hofu ni kuwa katika jamii zetu magonjwa haya yanaanza katika umri wa mapema zaidi na hivyo kuzorotesha nguvu kazi na kusababisha vifo katika umri chini ya miaka 60”.

Amesmea kuna mambo muhimu sana ya kuzingatia ili tudhibiti magonjwa haya ikiwemo ulaji wa vyakula unaofaa kwa kula mlo kamili, kuepuka vyakula pamoja na vinjwaji vyenye chumvi nyingi na sukari, kupungua unywaji wa pombe na kupunguza kula vitu vyenye mafuta.

Pia, amesema inatakiwa kujenga tabia ya kufanya mazoezi, kufanya uchunguzi wa Afya angalau mara moja kwa mwaka, upimaji wa Macho, Kisukari na magonjwa ya Moyo.

“Tukizingatia haya tutaweza kujikinga na magonjwa ambayo yanagharimu vifo vingi kwa watanzania na matumizi ya fedha nyingi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.” Amesema Bw. Mmuya

“Maonyesho haya ni muhimu sana kwa sababu yanawapa fursa wananchi kuweza kujifunza na kutambua kazi na huduma mbalimbali ambazo zinazofanywa na Wadau katika kupambana na kuzuia Magonjwa Yasiyoambukiza hapa nchini.” Amesema Bw. Mmuya

Mwisho, Bw. Mmuya amewakumbusha wananchi kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa UVIKO 19 kwa kuchanja na kuchukua hatua mbalimbali za kujikinga na hasa ukizingatia katika kipindi hiki kuwa na tishio la Ebola.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi-Magonjwa Yasiyoambukiza Dkt. James Kiologwe amesema Magonjwa hayo yataendelea kuongezeka kama tusiposhirikiana kwa pamoja kuyadhibiti.

“Watu kutotambua kama wana magonjwa yasiyoambukiza ni tatizo ambalo linasababisha kuongeza tatizo jingine, tushirikiane kwa kuwafikia walipo, kutoa elimu na kuwapima ili wajitambue.” Amesema Dkt. Kiologwe

Dkt. Kiologwe amesema ni muhimu kuwashirikisha wakinamama ambao wao ndio wana uwezo mkubwa wa kuzuia au kuongeza tatizo la magonjwa yasiyoambukiza katika vizazi vijavyo.

“Niwashukuru sana wadau wetu kwa kuendelea kuwa pamoja na Serikali hasa katika kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza nchini.” Amesema Dkt. Kiologwe

#MtuNiAfya
#JaliAfyaYako

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here