Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.
Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Macklina Komba akimfanyia usajili mwananchi wa Mkoa wa Geita aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.
Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) John Daniel akimpima Shinikizo la damu mkazi wa Chato aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kulwa Richard akimpima wingi wa sukari mwilini mkazi wa Chato aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyowakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali hiyo.