Home SPORTS YANGA KUKIPIGA NA CLUB AFRICAN SHIRIKISHO

YANGA KUKIPIGA NA CLUB AFRICAN SHIRIKISHO

Na: Mwandishi Wetu.

MABINGWA wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga wamepangwa kucheza na klabu ya Club Africain ya Tunisia katika mchezo wa Hatua ya Mtoano Kombe la Shirikisho Barani Afrika kupitia Droo iliyopangwa leo Oktoba 8,2022.

Yanga imeangukia katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika, baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Mabingwa wa Soka nchini Sudan Al Hilal, iliyoibuka na ushindi wa jumla wa 2-1.

Mchezo wa Mkondo wa kwanza utashuhudia Yanga ikicheza nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam, Novemba 02, ambapo mchezo wa marudiano utachezwa kwenye Uwanja wa Olympique de Radès uliopo mjini Tunis Novemba 09.

Hata hivyo ni mara ya pili msimu huu kwa Club Africain ya Tunisia kuja Tanzania, baada ya kucheza na Kipanga FC ya visiwani Zanzibar katika mchezo wa Hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.

Mchezo wa Mkondo wa kwanza ikicheza dhidi ya Kipanga FC kwenye Uwanja wa Amaan Unguja, Club Africain iliambulia sare ya bila kufungana, na iliporejea nyumbani kwao Tunisia kwa ajili ya Mkondo wa Pili, ilipata ushindi mnono wa 7-0.

Previous articleWAZIRI MKUU: SIJARIDHISHWA NA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA NAMTUMBO
Next articleBENKI YA DUNIA YAIPONGEZA TANZANIA KWA KUSIMAMIA VIZURI UCHUMI WAKE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here